ALIYOYASEMA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA HAFLA YA UAPISHO WA VIONGOZI WATEULE ILIYOFANYIKA TAREHE 5 JULAI, 2024 – ZANZIBAR
Zanzibar
WIZARA YA MADINI
#Nimefurahi kukujua leo maana nilikuwa nakusikia tu hongera kwa kuwa Katibu Mkuu. Waziri yuko pale najua mtakwenda kufanya vizuri. Wewe nimekutoa Tume ya Madini maana niliambiwa umefanya kazi nzuri sana, kwa hiyo nafasi yako ya Katibu Mkuu unaijua Tume vizuri najua utaisimamia vizuri.
#STAMICO tumefanya uwekezaji mkubwa sana na wamefanya vizuri, walipata zawadi kutokana na kufanya mageuzi makubwa na hata kwenye utoaji wa gawio kwa Serikali kwa hiyo nenda ukawasimamie vizuri shirika lisonge mbele.
#Kinachoniumiza kichwa ni kwenye leseni, mmetoa leseni nyingi watu wameshikilia lakini hakuna uwekezaji hakuna chochote kinachoendelea, nenda kalisimamie hilo. Waziri na mwenzie walishaanza kuangalia nani amefanya nini, nani ana nia na ana uhalali gani, nenda kalisimamie hilo.
#Sasa hivi nimetoka kuzungumza na Rais wa Benki ya Uwekezaji wa Europe (Ulaya) ananiuliza vipi huko madini kuna nini? Nimemwambia tumefanya utafiti wa kina kwa asilimia 16 tu kwa nchi nzima kama mnaweza mtusaidie kwenye hilo ili tujue tuna nini kwa kiasi gani. GST iongezewe nguvu ifanye tafiti za madini maeneo yote.
#Wachimbaji wadogo huko nyuma tulikuwa tunawaona kama kero lakini wameibeba Sekta. Juzi niliona taarifa ya kutoroshwa kwa madini ya dhahabu kutoka Afrika ya zaidi ya dola bilioni 35. Nenda kasimamie mapato ya dhahabu yarudi nchini, hatuna sababu ya kulia kwa kukosa dola.
#Hitimisho, ninawapongeza na ninawapa pole kwa kuamininiwa, mkafanye kazi kama Sheria zinavyotaka uongozi ni dhamana.
#InvestInTanzaniMiningSector
#Vision2030:MadininiMaisha&Utajiri
Social Plugin