Afisa mradi wa Afya Hatua anayehusika na huduma za kinga za saratani ya mlango wa kizazi , THPS mkoa wa Shinyanga, Aminael Tesha akitoa elimu kwa akina mama kuhusu saratani ya mlango wa kizazi waliotembelea banda la THPS - Picha na Kadama Malunde
Huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi zikiendelea katika banda la THPS
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wanawake Mkoa wa Shinyanga wamejitokeza kwa wingi kupata elimu pamoja na kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi inayotolewa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwenye Maadhimisho ya Siku ya Afya Mkoa wa Shinyanga yaliyopewa jina la Afya Code Clinic yaliyoratibiwa na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Jambo Fm kuanzia Julai 24 – 27,2024 katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.
THPS inashiriki katika maadhimisho hayo kwa kutoa elimu ya afya, upimaji VVU, afua za kinga, Tohara Kinga kwa wanaume na uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi.
Kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Misaada ya UKIMWI (PEPFAR) kupitia Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (U.S. CDC), THPS inatekeleza afua mbalimbali za afya ikiwemo huduma za afya ya uzazi na uzazi.
Baadhi ya akina mama walionufaika na huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi akiwemo Rose John na Tabitha Mipawa wameishukuru THPS na serikali kwa kuwapatia huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi ambapo wamefanikiwa kujua hali zao za afya na kuwashauri wanawake wengine kujitokeza kufanyiwa uchunguzi ili kuchukua hatua za mapema endapo watabainika kuwa na dalili za saratani hiyo.
Rose John akiishukuru THPS na serikali kwa kuwapatia akina mama huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi
Afisa mradi wa Afya Hatua anayehusika na huduma za kinga za saratani ya mlango wa kizazi , THPS mkoa wa Shinyanga, Aminael Tesha amesema maadhimisho ya Siku ya Afya Mkoa wa Shinyanga yamekuwa na manufaa makubwa kwani wanawake wengi wamefika katika banda la THPS kupata elimu pamoja na kufanyiwa uchunguzi wa saratani hiyo.
“THPS pamoja na watoa huduma kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga tunatoa elimu kuhusu saratani ya mlango wa kizazi na mama anaporidhia tunamfanyia uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi. Endapo tukikuta mama ana dalili za awali tunampa matibabu hapa hapa bandani kwetu, na iwapo atakuwa amevuka dalili za awali tutampa huduma endelevu kwa kumpa rufaa Hospitali ya Mkoa; na iwapo tutamkuta ana viashiria vya saratani ya mlango wa kizazi tutachukua sampuli na kuzipeleka Hospitali ya Rufaa Bugando kwa ajili ya uchunguzi zaidi,”amesema Aminael.
Afisa mradi wa Afya Hatua anayehusika na huduma za kinga za saratani ya mlango wa kizazi , THPS mkoa wa Shinyanga, Aminael Tesha
“Kupitia huduma hii akina mama wanapata elimu na kuondokana na imani potofu kwamba vipimo vya saratani ya mlango wa kizazi haviumi. Saratani ya mlango wa kizazi inatibika iwapo utawahi kufanya uchunguzi kwa hiyo naomba akina mama wote tuwe mabalozi kwa akina mama wenzetu, waambieni kuwa huduma hizi zipo uwanjani na kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya, waje wachunguzwe iwapo watabainika wana matatizo basi watapata tiba kulikoni kuacha kuja kuchunguzwa unakuja tayari tatizo limeshakuwa katika hatua mbaya”,ameongeza Aminael.
Naye Afisa Mradi wa Kupambana na saratani ya Mlango wa Kizazi na Ukatili wa Kijinsia Mkoa wa Shinyanga kupitia THPS, Dkt. Theobald Njoyo amesema Saratani ya mlango wa kizazi inaua hivyo amewaomba wanawake wajenge tabia ya kupima afya zao kwani saratani nyingi zikiweza kufanyiwa uchunguzi wa awali zinatibika na isipotibiwa mapema ni ngumu kutibika.
Afisa Mradi wa Kupambana na saratani ya Mlango wa Kizazi na Ukatili wa Kijinsia Mkoa wa Shinyanga kupitia THPS, Dkt. Theobald Njoyo.
“Katika banda hili mwitikio wa wanawake kuja kujua hali ya afya zao ni mkubwa, Julai 25 hadi 26,2024 tumepima wateja 120 na kati yao akina mama 8 mpaka sasa ni wahisiwa wa saratani ya mlango wa kizazi na tumewatibu na mmoja tumemkuta na dalili za saratani ya mlango wa kizazi na tumechukua sampuli kwa ajili ya vipimo zaidi Bugando”, ameeleza Dkt. Njoyo.
Amebainisha kuwa katika kipindi cha miezi tisa (Oktoba 2023 hadi Juni 2024), kupitia THPS wapokea huduma 21,759 walipimwa saratani ya mlango wa kizazi, ambapo 563 waligundulika kuwa na viashiria vya saratani hiyo na 552 kati yao walipatiwa matibabu.
Afisa mradi wa Afya Hatua anayehusika na huduma za kinga za saratani ya mlango wa kizazi , THPS mkoa wa Shinyanga, Aminael Tesha akitoa elimu kwa akina mama kuhusu saratani ya mlango wa kizazi waliotembelea banda la THPS
Afisa mradi wa Afya Hatua anayehusika na huduma za kinga za saratani ya mlango wa kizazi , THPS mkoa wa Shinyanga, Aminael Tesha akitoa elimu kwa akina mama kuhusu saratani ya mlango wa kizazi waliotembelea banda la THPS
Afisa mradi wa Afya Hatua anayehusika na huduma za kinga za saratani ya mlango wa kizazi , THPS mkoa wa Shinyanga, Aminael Tesha akitoa elimu kwa akina mama kuhusu saratani ya mlango wa kizazi waliotembelea banda la THPS
Afisa Mradi wa Kupambana na saratani ya Mlango wa Kizazi na Ukatili wa Kijinsia Mkoa wa Shinyanga kupitia THPS, Dkt. Theobald Njoyo akielezea kuhusu huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi
Tabitha Mipawa akiishukuru THPS na serikali kwa kuwapatia akina mama huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi
Huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi zikiendelea katika banda la THPS
Social Plugin