Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANANCHI NA VIONGOZI, WALALAMIKIA MKANDARASI WA TAKA

Lori lenye takataka lililoachwa Mtaa wa Mtambani, Tabata jijini Ilala tangu Jumamosi na kusababisha malalamiko kutoka kwa wananchi na viongozi wao.

Na Editha Majura,  Dar es Salaam.

MKANDARASI anayeondoa takataka Mtaa wa Mtambani, PB Urasa Logistics, Dar es salaam analalamikiwa kwa kutoondoa takataka kwa wakati, licha ya kuwatoza fedha kila mwezi.

Wakizunguza kwanyakati tofauti wakazi hao wameshangazwa na mkandarasi huyo kuacha gari lenye taka barabarani kwa zaidi ya siku tano, baada ya kuharibika.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Brighter Nchimbi amesema gari hilo lilionekana eneo lenye makazi ya viongozi, kwenye nyumba za Azimio likiwa na takataka na kwamba licha ya kumtaka Meneja wa  kampuni hiyo, Adam kuliondoa au kufaulisha taka hizo mpaka wakati akizungumza nasi hakuwa amefanya hovyo.

"Nimechoshwa na kero za hawa watu hata kwenye mkutano wa mtaa tulimuita Adam (meneja) wananchi wakampa kero zao lakini hawajirekebishi,” anasema Nchimbi.

Mfaume Towfique, mkusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa niaba ya Kampuni hiyo, akizungumza nasi jana - 09 Julai 2024 alikiri kuchelewa kutoa taka, akaahidi mabadiliko kwa sababu changamoto hiyo ni miongoni mwa sababu za yeye kuhamishiwa Mtaa huo.

Pia akakiri kufahamu kuwa gari lenye taka limebakia barabarani tangu Jumamosi, kwamba liliharibika Ingjini na kwamba jana - 09 Julai 2024 aliomba gari jingine ili takataka zifaulishwe.  

Hatahivyo leo asubuhi – 10 Julai 2024 gari hilo limekutwa na takataka ndani yake huku Meneja Adamu akihoji kama kuna mtu anakerwa na uwapo wa hali hiyo, kwamba taka hizo zimepuliziwa dawa, hazitoi harufu mbaya.

 Anasema wanaendelea kulitengeneza, likitengemaa litaondolewa kati ya leo au kesho asubuhi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com