Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DK. TULIA ATOA MISAADA WA UJENZI KITUO CHA POLISI MORO


 
Na Christina Cosmas, Kilombero

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU)ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya Tulia Trust ,Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ametoa msaada wa vifaa vya ujenzi  kwa Jeshi la Polisi wilaya  ya Kilombero Ili kumalizia ujenzi wa jengo la kituo Cha Polisi Kata ya Ching'anda.

Katika hafla Hiyo iliyofanyika Julai 26  mwaka huu 2024,Dkt. Tulia amemkabidhi nyumba ya kuishi Mzee Ambalile Mwala (74) ambaye amekuwa akiishi katika mazingira magumu pamoja na familia yake katika Kata ya Ching'anda Mlimba Mkoani Morogoro. Nyumba hiyo imejengwa na taasisi ya Tulia Trust.

Pamoja na hayo, Dkt. Tulia ametoa msaada wa madaftari, kiti mwendo kwa wahitaji na malumalu kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Kata ya Ching'anda Halmashauri ya Mlimba Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.

 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com