WEREMA ACHAGULIWA KWA KISHINDO MWENYEKITI MPYA UVCCM MKOA SHINYANGA


Bernard Benson Werema akishangiliwa baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Shinyanga.

Matokeo 

1. Benard Benson Werema - 252
2. Makamba Mussa Lameck - 78
3. Irene Nkooba Masakilija -  19
4.  Severine Leonard Mbulu - 12


Wagombea.


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga imefanya uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, ambapo Benard Benson Werema ameibuka Mshindi kwa kupata kura 252.

Uchaguzi huo umefanyika leo Julai 4,2024 na kusimamiwa na Mkuu wa wilaya ya Rorya Juma Chikoka.
Mwenyekiti Mpya UVCCM Shinyanga,Benson Werema 

Mchopanga akitangaza Matokeo hayo, amesema Wagombea walikuwa Wanne, kura zilizopigwa ni 367, kura zilizoharibika ni 6, huku kura halali ni 361.

Amemtaja Benard Benson Werema kuwa ndiyo Mshindi wa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, kwa kupata kura 252,Mshindi wa pili ni Makamba Mussa Lameck amepata kura 78, akifuatiwa na Irene Nkooba Masakilija kwa kupata kura 19, huku Severen Mbulu akipata kura 12.
Mkuu wa wilaya ya Rorya Juma Chikoka

Aidha,Werema akizungumza mara baada ya kupata ushindi huo amewashukuru Wajumbe kwa kumpigia kura na ameahidi atafanya kazi kwa bidii na kukipigania Chama Cha Mapinduzi ikiwamo kupata ushindi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na uchaguzi Mkuu mwakani.

Naye Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo, amepongeza uchaguzi huo kwa kufanyika kwa amani na utulivu, huku akiwasihi Vijana kwenda kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.
Pia,amewahamasisha Vijana wa UVCCM kwamba wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi za uongozi na ujumbe kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika mwaka huu.


Aidha, uchaguzi huo umefanyika mara baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Clement Madinda kujiuzulu nafasi hiyo mara baada ya kupata kazi mkoani Mbeya.

CHANZO - SHINYANGA PRESS CLUB BLOG



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post