Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa kihuduma DAWASA - Bagamoyo imewakumbusha wateja na Wananchi wanaotumia huduma za Maji kulipa ankara kwa wakati ili kuwezesha Mamlaka kuboresha huduma zake.
Rai hiyo imetolewa na Meneja DAWASA Bagamoyo, ndugu Christian Kaoneka wakati wa kukamilisha kwa zoezi la usomaji wa bili za mwezi Julai.
"Kila mteja ana wajibu wa kulipa ankara yake ya maji kwa wakati kulinganana na matumizi yake ya mwezi husika. Leo, Julai 15 tumehitimisha zoezi la usomaji wa Mita na wateja wameshaanza kupokea bili kupitia ujumbe mfupi hivyo tunawakumbusha kulipa bili kwa wakati." amesema
Mkoa wa Kihuduma DAWASA-Bagamoyo inahudumia wateja takribani 1640 katika kata saba za Zinga, Kiromo, Dunda, Nianjema, Kisutu, Magomeni na Yombo.
Social Plugin