Mtu mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano dhidi ya serikali huku wito wa kumtaka Rais William Ruto ajiuzulu ukiongezeka.Licha ya kuwa idadi ya waandamanaji haikuwa kubwa kama ilivyoshuhudiwa katika maandamano ya awali, kunao waliojeruhiwa, na kulazimika kutafuta matibabu ya dharura. hali hii ya polisi kukimbizana na waandamanaji ilidumu kutwa nzima.
Hapo jana Rais William Ruto alishtumu shirika la ford foundation la kimarekani kwa kufadhili maandamano nchini Kenya, tuhuma ambazo shirika hilo, limejitenga nazo.
Baada ya kulivunja baraza la mawaziri na kujiuzulu kwa Inspekta Jenerali wa Polisi wiki jana, waandamanaji bado wanasema Rais, hajatimiza masuala wanayodai yafanyiwe kazi ikiwemo suala la kuunda tume ya uchaguzi IEBC, kupunguza idadi ya wizara katika serikali yake kutoka 22 hadi 15, pamoja na kuwachukulia hatua Maafisa wa Usalama wanaotuhumiwa kuwauwa waandamanaji.
Social Plugin