Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BABU WA MIAKA 70 MATATANI KWA KUBAKA MTOTO


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Manyara George Katabazi

Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara linamshikilia Mohamed Omary mzee mwenye umri wa miaka 70 mkazi wa kijiji cha Kiru mkoani Manyara kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye ulemavu wa miguu wa miaka 11 wakati akiwa nje ya nyumba yao.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Manyara George Katabazi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo majira ya jana asubuhi Julai 2, 2024, na kusema kuwa timu ya uchunguzi ipo katika eneo hilo kufanya uchunguzi ili kubaini sababu ya ukatili huo uliofanyika kwa mtoto huyo.

Wananchi nao hawakuwa mbali kutoa hisia zao kuhusu tukio la ubakaji lililofanyika kwa mtoto huyo.

CHANZO - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com