BABA LEVO ATUA SHAMBANI KWA MR. MANGURUWE... "KWELI NGURUWE WENGI WAPO,NJOONI MUWEKEZE"


Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Mtangazaji na Msanii wa kizazi kipya kutoka Wasafi Media Baba Levo ametembelea Kijiji cha Nguruwe kilichopo Zamahero Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kujionea uwekezaji mkubwa unaofanywa na Mkurugenzi wa Kijiji cha Nguruwe Project Simon Mkondya Maarufu kwa jina la Mr Manguruwe.

Baba Levo ametembelea Mradi huo mkubwa wa ufugaji Nguruwe leo Jumapili Julai 14,2024 akiwa ameambatana na waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali ili kujionea mradi huo ambao umekuwa gumzo kila mahali.

Katika mazungumzo na waandishi wa habari akiwa katika mradi huo Baba Levo amesema amekwenda kujionea kwa macho kuhusu uwekezaji wa Mr. Manguruwe lakini kumwakilisha Msanii Shilole yeye kama kaka ambapo mara kwa mara Mr. Manguruwe amekuwa akimhitaji kuwa mke wake. 

"Tumekuja kujihakikishia  kuwa je yale ambayo amekuwa akiyasema hapa Dodoma yamo?, tumeambata na Vyombo vya habari nyingi sana katika hii ziara. Nimejionea maajabu ya Kijiji cha Nguruwe.... Tumeona kweli nguruwe wapo, mabanda ni mengi na mengine yanaendelea kutengenezwa, lakini mifumo ya kisasa imefungwa kwa ajili ya kuwalinda nguruwe.

Watanzania karibuni kwa Mr. Manguruwe mpate nguruwe wa kisasa kwa ajili ya chakula lakini pia mpate nguruwe wa kisasa kwa ajili ya kufuga", amesema Baba Levo.
Kwa upande wake, Mr. Manguruwe ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wadau mbalimbali  kuwekeza katika ufugaji wa nguruwe kwenye mradi huo na kupata faida.

"Sasa kuna fursa kubwa kwako wewe ya uwekezaji katika ufugaji wa nguruwe Tanzania.  Karibu uwekeze kuanzia shilingi Milioni moja ili ufugiwe nguruwe na upate faida kila siku ya shilingi 10,000/= kwa miezi sita kwa mfumo wa Rent to Own (Azima Umiliki). Ofisi zetu zipo Dar es salaam nyuma ya PSSF  Tower mtaa wa Super Star Ofisi namba 15. Kwa Arusha jengo refu kuliko yote la Ngorongoro Tourism Tower ghorofa ya 2 na Dodoma pale Dodoma Hotel au Shambani Zamahero Bahi Dodoma.

 Au tupigie kwa simu namba +255623200100 au +255757007200",amesema Mr. Manguruwe.

"Nguruwe waliopo hapa ni Salama, ni wasafi wanaoshwa vizuri, hakuna nguruwe yeyote mwenye  ugonjwa wowote wala changamoto ya kiafya, hapa tuna maelfu ya nguruwe, tuna nguruwe wengine ni warefu",ameeleza Mr. Manguruwe.
Mtangazaji na Msanii wa kizazi kipya kutoka Wasafi Media Baba Levo amakiwa katika Kijiji cha Nguruwe kilichopo Zamahero Mkoa wa Dodoma akishuhudia uwekezaji mkubwa unaofanywa na Mkurugenzi wa Kijiji cha Nguruwe Project Simon Mkondya Maarufu kwa jina la Mr Manguruwe.


Mkurugenzi wa Kijiji cha Nguruwe Project Simon Mkondya Maarufu kwa jina la Mr Manguruwe akimweleza jambo Mtangazaji na Msanii wa kizazi kipya kutoka Wasafi Media Baba Levo (kulia) alipotembelea Kijiji cha Nguruwe kilichopo Zamahero Mkoa wa Dodoma 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post