Hayo yameelezwa na wadau katika kikao cha tathimini ya utekelezaji wa programu ya uchechemuzi wa sheria za habari Zanzibar kilichowashirikisha waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kisiwani Pemba.
Zaina Mzee ambaye ni afisa programu hiyo kutoka TAMWA ZNZ, amesema program ya uchechemuzi wa mabadiliko ya sheria za habari zinazokwaza uhuru wa habari Zanzibar imeonyesha kuleta mabadiliko ya maboresho kwenye baadhi ya vifungu vya sheria za habari ambazo ni kandamizi.
Alieleza, kupitia programu hiyo tayari TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Kamati ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar ZAMECO wamefanya vikao na taasisi za serikali ambazo zinahusika na utungaji wa Sheria kwaajili ya maboresho ya vifungu vya Sheria husika.
Alieleza, "kupitia mradi huu tumefanya vikao vingi na wadau wa Sheria ikiwemo tume ya kurekebisha Sheria, wajumbe wa Baraza la wawakilishi, NGOs pamoja na wandishi wa habari unguja na Pemba.”
Akitoa maelezo ya tathimini ya vipindi, makaka na habari, Mohamed Khatib ambaye ni mtaalam wa tathimini na ufuatiliaji alisema shabari, makala na vipindi ambavyo vimetolewa vimeonyesha ni jinsi gani wandishi wamekuwa na uwelewa wa kutosha juu vifungu vya sheria ambavyo ni kikwazo kwao.
"Tumepokea makala nyingi kutoka kwenye social media, magazeti, na vipindi vya redio. Kwa kweli zimechambua Sheria na mapungufu pamoja na mapendekezo ya nini kifanyike ili kusiwe na vikwazo Kwa wandishi wa habari," alifafanua Mohammed.
Baadhi ya wandishi wakichangia wameushauri kuwa na mwendelezo wa uchechemuzi wa vifungu vinavyokwaza uhuru wa habari ili sheria hizo ziwee kufanyiwa marekebisho na kuwawezesha waandishi kutekeleza majukumu yao kwa uhuru.
Mwanddishi wa habari Masanja Mabula alieleza, “waandishi wa habari tunatakiwa tutumie fursa hii ya elimu tuliyopata ya kuzijua sheria na mapungufu yake kwa kuidi kuyaandikia mapungufu yaliyopo ili yafanyiwe marekebisho.”
TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na wadau wa habari ilifanya mapitio ya sheria nane (8) za habari zenye vifungu vinavyokwaza uhuru wa habari Zanzibar ikiwemo Sheria ya usajili wa wakala wa habari, magazeti na vitabu namba 5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria no.8 ya 1997, Sheria ya Tume ya Utangazaji Zanzibar namba 7 ya mwaka 1997 iliyorekebishwa na sheria namba 1 ya mwaka 2010.