KSIJ YAADHIMISHA SIKU YA ASHURAA

Na Hadija Bagasha Tanga

Madhehebu ya kiislamu jijini Tanga,  Koja Shia Ithna Asheri Jamaat Tanga (KSIJ)  chini ya Mwenyekiti wake Sameer Bandali yamejumuika kwa pamoja kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Ashuraa siku aliyouwawa kikatili mjukuu wa mtume,  Hussein Ibn Ally huku wakitumia siku hiyo kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kupinga ndoa za jinsia moja katika Mkoa Tanga. 

Akiongea wakati wa maadhimisho hayo yalifanyika jijini Tanga, Sheikh Shafii Mohamed Nina amesema waislamu wanaona umuhimu wa kumbukumbu ya  mjukuu wa mtume  kama kielelezo muhimu kwenye maisha yao ya sasa.

"Siku kama hii tunaiadhimisha Kwa sababu ni msiba mkubwa na ni jambo kubwa ambalo liliugusa uislamu na bahati mbaya liliugusa uongozi wa uislamu kwakuwa alikuwa Kiongozi na mtu mkubwa zaidi Duniani kipindi hicho"

"Kumbukumbu ya kuuwawa Al Imamu Husseni ina mambo mengi, kwanza namna aliyouwawa, wale waliomuua, na mazingira aliyouwawa, yanatufundisha mengi hasa katika uislamu na ubinadamu kwa ujumla", amesema.

Pamoja na mambo meingine waislamu wanatumia siku hii kuitaka jamii na dini zote kuungana na kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia, ikiwemo kupinga ndoa za jinsia moja.

"Kuhusu haya mambo ya ushoga, hiki kipindi tunachoishi sasa ndiyo hasa cha kuitumia dini zaidi kupambana na jambo hili kwakuwa hakuna suluhisho isipokuwa ni dini", amebainisha.

"Na dini zote za mbinguni zinapambana na jambo hili, na hata tukiishi katika jamii zetu za Kiafrika hali hii ni ngumu sana, dini zote ziamke kupambana ndiyo tuweze kuokoka kwa sababu tukiziangalia jamii zetu zinapotea",amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti KSIJ Tanga, Samir Bandal amesema tukio la kuuwawa Imamu Hussein limewafundisha mambo ambayo yapo kwenye maisha ya kila siku ya binadamu na kwamba uislamu ni amani na sio vita.

"Hii siku ya Ashuraa inatukumbusha kulinda Uislamu, kuishi kwa uhuru na amani lakini pia Imamu Hussein alikwenda Kalbara siyo kwa nia ya vita bali alifuata amani, amesema Bandal.

"Pia siku hii inatukumbusha kwamba Imamu wetu ametangaza amani pamoja na haki za binadamu, na tumefanya haya yote ili tuwakumbushe watu kwamba alitoa familia yake yote kutangaza mambo yote ya kumpendeza Mungu" ,amefafanua.

Kumbukumbu ya kifo cha Mjukuu wa Mtume Imamu Husen hufanyika kila mwaka wailamu wakikusanyika wakifanya matendo ya kibinadamu yaliyokuwa yakifanywa na mtume huyo wakati wa enzi ya uhai wake.








Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post