WATAKIWA KUWAFIKISHIA KWA WAKATI WAKULIMA WA PAMBA TEKNOLOJIA ZINAZOVUMBULIWA


Dk. Paul Saidia kutoka TARI Ukiriguru
Thomas Daudi mratibu wa pamba kitaifa

Na Christina Cosmas,  Morogoro

MAAFISA kilimo na ugani nchini wametakiwa kuwafikia wakulima wa Pamba na kutoa elimu matumizi ya teknolojia zinazovumbuliwa ili kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa wakulima.

Rai hiyo imetolewa na kaimu katibu tawala wilaya ya Ulanga Huluka  Hamisi wakati wa maadhimisho ya siku ya mkulima kupitia mradi wa Cotton Victoria yaliyofanyika wilayani Ulanga mkoani.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya UTafiti wa kilimo (TARI) Ukiriguru Dk. Paul Saidia amesema ipo haja kwa wakulima wa pamna kufuata ushauri wa kitaalamu ikiwemo kukatia shina mama ili kufanya zao hilo kukua na kuketa tija kwenye mavuno.

Awali mratibu wa zao hilo kitaifa Thomas Daudi ameyataja mafanikio yaliyoanza kujitokeza kutokana na upandaji wa kufuata ushauri wa kitaalam wa sentimita 60 kwa 30  kuwa ni pamoja na kupanda mimea mingi zaidi kuliko kupanda mpando wa kawaida ambao mimea yake huwa maichache na mavuno ni kidogo.

Nao baadhi ya wakulima wa Pamba wilayani humo akiwemo Adela Kamili waliishukuru serikali kwa kutuma wataalamu hao kuwapa elimu hiyo ambayo itawasaidia kuinuka katika kilimo cha zao la Pamba na kuzidi kukitegemea kama zao kuu la biashara kwao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post