Na Avelina Musa - Iringa
WAFUGAJI wa kuku na Nguruwe wameaswa kufuga kisasa ili wapate faida na kuondokana na umaskini.
Hayo yameelezwa na Meneja wa Kanda ya Kati Kampuni ya Feed Lance Intelligent Feeding Bw. Musab Mwenda katika semina iliyowakutanisha wafugaji wa kuku na Nguruwe Mkoani Iringa.
Musab amesema Kampuni hiyo inajihusisha na Usambazaji na Uuzaji wa Concentrate za kuku na nguruwe yenye Makao Makuu yake Nchini Uholanzi ambapo kwa Tanzania inatoa huduma hiyo katika Mikoa yote nchini.
Amesema lengo la Semina hiyo ni kuwaelimisha wafugaji namna ya kulisha mifugo katika njia iliyo bora na yenye tija na ulishaji wa kuokoa gharama.
"Kampuni hii imeona ni vyema kuwakuwatanisha wafugaji Hawa ili waweze kujua namna Bora ya kufuga kwa kufuata njia za kisasa na kupata mafanikio,"amesema.
Kwa Upande wake Mshiriki katika Semina hiyo Bi. Neema Andrew ameishukuru Kampuni ya Feed Lance Intelligent Feeding kwa kutoa Elimu kwa wafugaji wa Mkoa huo kwani wameongezewa maarifa ya kufuga kisasa na kwa tija.
Hata hivyo pamoja na semina hiyo wafugaji walipata nafasi ya kushiriki kuzungusha gurudumu ambapo walijishindia zawadi mbali mbali kutoka katika kampuni hiyo.
Semina hiyo ilikuwa na kauli Mbiu Isemayo "Teknolojia Mpya ya malisho yenye tija kwa wafugaji wa kuku na Nguruwe".