Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema suala la usalama wa kimtandao ni muhim ili kuhakikisha upatikanaji
Akizungumza wakati wa ziara yake makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) tarehe 18 Julai, 2024 Mhandisi Mahundi ameishukuru timu zima ya TCRA kwa
umahiri mkubwa katika usimamizi wa sekta hasa katika eneo la usalama mtandao.
Amesema, umahiri wa TCRA kunaifanya Wizara kuonekana inawajibika na kuendelea kulipa Taifa heshima huko duniani
ambapo mpaka sasa tupo katika nafasi nzuri kimataifa katika
masuala ya usalama mtandao.
Aidha, ametoa rai kwa TCRA kuendelea kukimbizana na
mabadiliko ya teknolojia kwa wataalam kujifunza na kuongeza
ujuzi mara kwa mara ili kuweza kukabiliana na wahalifu wa mtandaoni wanaoenda sambamba na kasi ya ukuaji wa teknolojia kwa kubuni mbinu mpya za kufanya uhalifu.
Mhandisi Mahundi amesema kuwa lengo la ziara yake ni kujifunza utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kumsaidia Mhe. Waziri Nape Nnauye ipasavyo lakini pia kuitendea haki nafasi adhimu aliyopewa na Mhe. Dkt. Samia ya kuwahudumia watanzania.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabir Kuwe amekiri
kuwa teknolojia inavyokuwa wahalifu pia hutafuta mianya na
mbinu mpya za kufanya halifu ambapo amebainisha chanzo
cha matukio ya uhalifu mtandaoni yanasababishwa na watu