Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BYABATO KUTOA KOMPYUTA MPAKATO KUKUZA TAALUMA



Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Wakili Stephen Lujwahuka Byabato anatarajia kutoa Kompyuta mpakato (LAPTOP) zipatazo 109 ili kuendelea kukuza kiwango cha Taaluma katika halmashauri ya Manispaa ya Bukoba

Katika jitihada za Kuunga Mkono Juhudi za Serikali katika Sekta ya Elimu kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Mbunge huyo atatoa kompyuta Mpakato (LAPTOP) kwa Watendaji wa kata, Waratibu kata, Wakuu wa Shule za Sekondari na Binafsi pamoja na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi za Serikali na Binafsi kulingana na Idadi yao Ili zisaidie katika jitihada za kuinua Kiwango Cha Elimu na Ufaulu kwa wanafunzi wa halmashauri ya Manispaa hiyo.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Mbunge Ndg. Pasaka Bakari wakati akichangia katika Majadiliano ya Kikao cha Wadau wa Elimu mkoani Kagera chini ya Mwenyekiti wake Hajat Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa Kagera, chenye lengo la Kutathimini kiwago cha Elimu na Kuweka mikakati ya kuongeza Kiwango Cha ufaulu.

Ndg. Pasaka aliyemuwakilisha Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Stephen Byabato Kutokana na udhuru ya Kikazi amesema kuwa Mbunge huyo Byabato anatarajia kukabidhi Laptop 109 kwa Wahusika hao kwa kila Kata pamoja na Shule hizo, Ili zisaidie katika Masuala ya kitaaluma.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com