Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CCM TANGA KUTUMIA MILIONI 35 KUWAPELEKA DARASANI MADEREVA DALADALA

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rajabu Abdurhaman akizungumza na wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Tanga akitokea Jijini Dodoma ambapo Kamati kuu ya CCM Taifa ilimteua katika nafasi hiyo.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rajabu Abdurhaman kushoto akizungumza na mmoja wa madereva  Daladala Jijini Tanga Husein Ramadhani na wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Tanga akitokea Jijini Dodoma ambapo Kamati kuu ya CCM Taifa ilimteua katika nafasi hiyo.

KATIBU wa CCM Mkoa wa Tanga Suleiman Senkwa akizungumza wakati wa mapokezi hayo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Burian akizungumza wakati wa halfa hiyo
Na Oscar Assenga, TANGA

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimehaidi kuwasomesha madereva wa Daladala Jijini Tanga 200 ambao itagharamia kiasi cha Milioni 35,000,000 kwa ajili ya kuwawezesha kupata elimu na leseni ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha ajali zinapungua.

Hayo yalisemwa leo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Rajabu Abdurhaman wakati akizungumza katika mapokezi yake yaliyofanyika kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Tanga akitokea Jijini Dodoma ambapo Kamati kuu ya CCM Taifa ilimteua katika nafasi hiyo.

Rajabu ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga alisema kwamba ameamua kufanya hivyo ili kuhakikisha madereva ambao wanaendesha vyombo vya usafiri wanapata ujuzi ili kuweza kuepuka ajali wanazoweza kukumbana nazo.

“Sheria zimekuja lazima madereva wasome kwa hiyo lazima msome kweli ili muweze kuwa na halali CCM kazi yake ni kuwaunga mkono vijana ili muweze kusoma hivyo nitawaunga mkono nikitambua kwamba nyie ni wadau muhimu kwenye usafirishaji”Alisema

“Kwa hiyo kama mlivyosema gharama ya kusoma ni 255,000 na nyie mnauwezo wa kutoa 100,000 niwaombe mjikusanye katika hiyo pesa kila mtu nitamuongezea 150,000 iliyobakia hivyo jumla nitatoa Sh.Milioni 35,000,000 kwa watu 200 ninawaunga mkono nikitambua nyie ni wada muhimu kwenye usafiishaji”Alisema

Aidha alisema kwamba watakapokuwa wamesoma na kuendelea kufanya shughuli zao itasaidia kupungunza ajali huku akieleza ameamua kufanya hivyo kwa sababu kama kiongozi wajibu wake ni kuisaidia jamii na hayo ni maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu kuwaunga mkono vijana kuweza kujikwamua kiuchumi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com