Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeendelea kutekeleza zoezi la ufuatiliaji wa malipo ya huduma za maji kwa wateja wa madeni ya muda mrefu na mfupi katika mkoa wa kihuduma DAWASA Kinondoni.
Zoezi hilo lina kwenda sambamba na utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya huduma ya maji, ulinzi wa miundombinu ya maji, pamoja na umuhimu wa kulipa bili za maji kwa wakati.
Ulipaji wa bili kwa wakati kutasaidia Mamlaka kuboresha zaidi huduma zake kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.
Social Plugin