Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amewaelekeza Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kutimiza wajibu wao kwa kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya Wananchi wanaowahudumia.
Waziri Aweso ameyasema hayo katika kikao kazikazi na Watumishi wa mikoa ya kihuduma DAWASA Mbagala na Temeke wakati wa muendelezo wa ziara yake ambapo ameelekeza uboreshaji wa huduma kwa wateja pamoja na kuongeza maunganisho ya huduma kwa wateja.
Mhe. Aweso anaendelea na ziara yake Mkoani Dar es salaam iliyolenga kukagua uzalishaji na usambazaji Majisafi pamoja na uhakika wa upatikanaji wa huduma kwa Wananchi
Social Plugin