Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, akipokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Cecil Francis, wakati alipotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (SabaSaba).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, akipokea zawadi kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) aliyokabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Cecil Francis, wakati alipotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (SabaSaba).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, akipokea maelezo ya huduma zinazotolewa na TTCL, kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Cecil Francis, wakati alipotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (SabaSaba).
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Sulemani Jafo akimkabidhi tuzo , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL) Bw. Cecil Francis, baada ya Shirika hilo kushika nafasi ya pili katika kipengele cha Sekta ya Mawasiliano nchini kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kwa mwaka 2024 ambayo yamehitimishwa leo Julai 13 .
Baadhi ya Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL) wakishangilia baada ya Shirika hilo kushika nafasi ya pili katika kipengele cha Sekta ya Mawasiliano nchini kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kwa mwaka 2024 ambayo yamehitimishwa leo Julai 13 .
Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi ametembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) na kupokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Cecil Francis.
Akiwa katika Banda hilo Rais Dk. Mwinyi alioneshwa huduma zinazotolewa na TTCL pamoja na mchango wa Shirika hilo katika sekta ya mawasiliano hapa nchini.
TTCL imetumia fursa hiyo pia kumuonesha Dk. Mwinyi maendeleo yaliyofikiwa katika utekelezaji wa majukumu ya Shirika kwa Wananchi ya kuhakikisha huduma za Mawasiliano inawakia kikamilifu.
Katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kwa mwaka 2024 ambayo yamehitimishwa leo Julai 13 , TTCL imeshika nafasi ya pili na kupata tuzo katika kipengele cha Sekta ya Mawasiliano nchini.
Maonesho hayo yamefungwa rasmi na Mheshimiwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi ambapo yalikuwa yakiongozwa na kauli mbiu isemayo "Tanzania: Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji,"
Social Plugin