Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Dkt. Doto Biteko akimkabidhi kombe la ushindi Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile baada ya EWURA kuibuka mshindi wa jumla katika Bonaza la Michezo liloandaliwa na Wizara ya Nishati likishirikisha Tassisi 11 zilizochini ya Wizara hiyo leo 27.7.2024 jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenister Mhagama.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe, Dkt. Doto Biteko,akizungumza na Watumishi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake waliposhiriki kwenye Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dkt. James Andilile,akizungumza mara baada ya EWURA kuibuka Mshindi wa Jumla katika bonanza hilo walioshiriki katika Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dkt. James Andilile,akishiriki mbio za kukimbia ambapo ameibuka mshindi wa kwanza katika mbio hizo wakati wa Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
.....
Leo tarehe 27 Julai 2024, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)imeibuka mshindi wa jumla wa michezo yote katika bonanza la michezo la Wizara ya Nishati lililofanyika viwanja vya Sekondari ya John Merlin, Miyuji Dodoma.
Michezo iliyofanyika kwenye Bonanza hilo ni riadha mita 100 (wanaume na wanawake), kupokezana vijiti (wanaume na wanawake), rede, karata, kukimbia na yai ndani ya gunia, kukimbia na maji kwenye glasi,kupenya ndani ya pipa, mpira wa miguu, mpira wa pete, bao na karata.
Mgeni rasmi katika bonanza hilo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Mashaka Biteko amewashauri watumishi wa Wizara na taasisi zake kuwa na desturi ya kufanya mazoezi ili kuimarisha na kulinda afya dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile aliishukuru Wizara ya Nishati kwa kuandaa bonanza hilo na kusema kuwa limeleta utangamano miongoni mwa viongozi na wafanyakazi walioshiriki.
Social Plugin