FCC KUHAKIKISHA WANANCHI HAWAUMIZWI NA BIDHAA BANDIA


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

TUME ya Ushindani nchini (FCC) imeendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuhusu bidhaa bandia katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho hayo leo Julai 3, 2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa FCC, William Erio amesema FCC itahakikisha mwananchi nchini haumizwi na bidhaa zisizo na ubora ikiwemo kusimamia sheria ya ushindani nchini inayodhibiti bidhaa hizo.

Aidha Erio amesema FCC imejitahidi kutoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya kuepuka bidhaa bandia.

"Majukumu yetu pia ni kutoa elimu kwa watu kutofanya Biashara Bandia na kuhalibu ushindani wa biashara,sisi FCC tutaendelea kuchukua hatua"amesema Erio.

Pamoja na hayo amewataka wafanyabiashara na wawekezaji kabla ya kufanya biashara nchini watembelee FCC kwa lengo la kupata elimu .

"Na sisi tunatumia maonesho haya pamoja na kueleza kazi kwa Umma,tunatumia maonesho haya pia kunawashauri kutofanya Biashara Bandia pamoja kutoweka bei kubwa itakayomuumiza mlaji,"

"Tunawakaribisha kwenye Banda hili ,na sisi tutatoa elimu kipindi chote cha maonesho"Amesema Erio.

Hata hivyo, amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania ni sehemu sahihi kwa uwekezaji kutokana na sera nzuri ikiwemo kuwepo kwa Mamlaka inayodhibiti bidhaa bandia ikiwemo FCC.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post