JESHI la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mtwara limefanikiwa kuokoa vibanda 211 katika moto uliokuwa unawaka kwenye soko la Mkuti Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ambapo chanzo cha moto huo hakikujulikana.
Akizungumza mara baada ya tukio hilo Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mtwara, Mrakibu Oisa Singili amesema askari wa zamu walifika eneo la tukio na kufanikiwa kuudhibiti moto uliokuwa ukiwaka usilete madhara.
Aidha amesema kuwa chanzo cha moto huo kuwaka hakikuweza kufahamika mara moja na uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo ambapo asilimia kubwa ya vibanda vya biashara na mali zimeokolewa.
Social Plugin