Na Ferdinand Shayo ,Manyara
Kampuni ya Mati Super Brands Limited inayozalisha vinywaji changamshi iliyopo mjini Babati Mkoani Manyara imedhamini timu ya mpira wa miguu inayoshiriki ligi kuu ya soka tanzania bara ya Fountain Gate kupitia kinywaji chake kipya cha Tanzanite Royal Gin ambapo timu hiyo imeingia makubaliano ya udhamini wa mwaka mmoja na kampuni hiyo .
Akizungumza katika Halfa ya kusaini mkataba wa udhamini Huo,Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema kuwa wameamua kudhamini timu hiyo ili kutoa fursa kwa wakazi wa Mkoa wa Manyara kupata burudani ya soka kutoka kwa timu ya Fountain Gate na kunufaika na fursa za uwepo wa timu hiyo na timu mbalimbali zitakazofika mkoani hapa ikiwemo wafanyabiashara,wajasiriamali .
Mulokozi amesema kuwa uwepo wa timu hiyo utachochea maendeleo ya michezo mkoani Manyara Pamoja na maendeleo ya kiuchumi kutokana na timu hiyo kupiga kambi mkoani Manyara .
“Leo Tumewaletea Habari Njema kwa mkoa wa Manyara kuwa timu hii pendwa ya Fountain Gate imehamia Mkoani Manyara chini ya Udhamini wa Kampuni ya Mati Super Brands Limite kupitia kinywaji kipya cha Tanzanite Royal Gin” Anaeleza David Mulokozi Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited.
Mkurugenzi wa Timu ya Fountain Gate Japhet Makau ameishukuru Kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa udhamini mnono na kuahidi kufanya vizuri katika mashindano mbali mbali ya kitaifa na kimataifa.
Afisa Mtendaji Mkuu Timu ya Fountain gate kidawawa thabita amesema wachezaji wote wana hali nzuri na wako tayari kushiriki mashindano wakati wowote na kuongeza kuwa udhamini huo utaongeza ufanisi mkubwa kwenye timu hiyo.
Social Plugin