Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KINANA AWASHAURI VIONGOZI CCM KUZINGATIA MAADILI



Na mwandishi wetu, Katavi

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Abdulrahman Kinana amewashauri viongozi wa CCM wa ngazi mbalimbali kuwa mfano bora wa maadili na malezi mema.

Ameeleza hayo leo Julai 11, 2024 alipofungua Kongamano la Malezi na Maadili lililondaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama, mjini Mpanda, mkoani Katavi.

“Sisi viongozi tunatakiwa kuwa mfano wa maadili na hasa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kwa kuepuka mambo yote ambayo yataleta sifa mbaya kwa Chama au kuleta sifa mbaya kwa wana CCM na viongozi wake.

“Tunawajibu wa kuyasimamia maaadili, maadili ni mambo yote mema na kueupka mabaya. Sisi viongozi ndani ya CCM tunatakiwa wakati wote kuwa mfano kwa kauli zetu na vitendo vyetu kwa maisha yetu yote.Tuwe mfano wa uadilifu, kila anayekuona uwe tafsri ya maadili, tuwe tafsiri ya sifa za uadilifu,” ameema.

Kwa mujibu wa Kinana, CCM imeendelea kuwa chuo cha maadili ndio maana kumekuwa na Kamati za kusimamia maadili katika ngazi zote kuanzia chini hadi Taifa.

Amesisitiza kuwa kauli zinazotolewa na viongozi mbalimbali zinadhihirisha maadili, kukemea rushwa, mambo yasiyo mema kwa jamii na kuhimiza kujenga undugu, mshikamano na kusaidiana.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com