LIGI YA BYABATO BUKOBA CUP YAZINDULIWA RASMI NA NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI , SANAA NA MICHEZO.

Naibu waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma akizungumza  wakati wa uzinduzi wa Ligi ya Byabato Bukoba Cup wakati alipokuwa mgeni Rasmi.
Naibu waziri wa Utamaduni , Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma akisalimiana na  Marefa pamoja na wachezaji wakati wa uzinduzi wa Byabato Bukoba Cup
Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Adv Stephen Byabato(Aliyevaa Tshirt Nyeusi)  ambaye ndiye muandaaji wa Ligi ya Byabato Bukoba Cup

Na Mariam Kagenda - Kagera

Wizara ya utamaduni,sanaa na michezo nchini tayari imeanza hatua ya kutafuta vipaji kupitia michezo mbalimbali inayoendelea zikiwemo ndondo Cup ili kukuza vipaji ajira,ushirikiano pamoja na mahusiano.

Naibu Waziri Wizara ya Utamaduni,sanaa na Michezo Hamis Mwijuma amesema hayo Julai 06,2024 wakati akizindua ligi ya Byabato Cup ya Mbunge wa jimbo la mjini Wakili Stephen Byabato Mkoani Kagera ambapo amesema serikali ya awamu ya sita kwa inatambua umuhimu wa michezo ikiwa ni njia moja wapo ya kuboresha afya na kuoneka kama kazi nyingine maana vijana wengi wameajiriwa katika sekta za burudani na michezo kupitia hapo wemekuwa matajiri wakubwa jambo ambalo linakuza uchumi na maendeleo ya Nchi.

"Mhe. Rais ametupatia kazi hiyo ya kusaka vipaji kote nchini niwahakikishie kwenye ligi hii nitaleta skauti hapa ili kuangalia vijana wenye vipaji na tuhakikishe tunawapeleka kwenye timu kubwa waweze kuhudumia nchi hii"amesema Naibu waziri Mwijuma.

Katika hatua nyingine Naibu waziri Mwijuma amesema mwaka 2027 Tanzania inaandaa mashindano ya Afcon kwa kushirikiana na nchi za Kenya na Uganda kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi tunafanya marekebisho makubwa kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa,Amani na tunajenga uwanja wa Samia Suluhu Hassan Arusha huku tutaendelea kufanya marekebisho katika viwanja mbalimbali na mchakato huo utafika kaitaba stadium kwa juhudi za Mhe, Rais Samia.

Ligi ya Byabato Cup imeanza kutimua vumbi julai 06 mwaka 2024 ikishirikisha timu 14 za kata zote ambapo mechi ya awali ilikutanisha timu za wanawake Victoria Queen's dhidi ya Omiseta Queen's mpaka dakika tisini zinatamatika za maamuzi wa kati Geturuda Gerevazi zimetoka sale ya goli mbili na Mchezo wa ufunguzi wa jioni umekutanisha timu ya Bilele na Bakoba.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini wakili Stephen Byabato amemshukuru Naibu waziri wa Utamaduni ,Sanaa na Michezo Hamis Mwijuma kwa kuzindua ligi hiyo ambayo itakuwa msaada mkubwa wa kichocheo cha michezo kwa wakazi wa Bukoba.

Amesema kuwa yy kama kiongozi anatambua umuhimu wa michezo kwa kukuza vipaji na upande wa ajira pia ndo maana ameamua kuweka ligi hiyo na kuongeza kuwa ataendelea kuwasaidia vijana kuinua vipaji vyao .

Katika ligi hiyo ya Byabato Bukoba Cup mshindi wa kwanza atapata kiasi cha shilingi Milioni 3, wa pili Milioni 2 na wa 3 Milioni 1

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post