MALAMBA MAWILI WAPOKEA VIFAA KUKAMILISHA MRADI WA MAJI KWEMBE


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imetekeleza agizo la Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso la kuhakikisha wakazi wa Kata ya Kwembe na Msigani katika Wilaya ya Ubungo kwa vifaa vya mradi vya thamani ya Shilingi milioni 257.

Akiongea katika makabidhiano hayo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mhe. Issa Mtemvu ameishukuru Wizara ya Maji kupitia DAWASA kwa utayari wa kutekeleza mradi wa maji Kwembe utakao kuboresha upatikanaji wa maji kwa wakazi takribani 10,000 wa Kata za Kwembe na Msigani.

Utekelezaji wa mradi unatarajia kukamilika mwisho wa Mwezi Julai mwaka huu utanufaisha wakazi mitaa ya Kwembe, Kwembe Mpakani, King'azi A, Njeteni, Msigani, Malamba mawili na Kwa Hakimu.

Mradi wa Kwembe umehusisha utoaji wa toleo kwenye bomba la inchi 16 linalopeleka maji katika mji wa Kisarawe na ulazaji wa bomba za inchi 8 kwa umbali wa kilomita 3.5 ambapo hadi sasa bomba zimelazwa kwa umbali wa kilomita 2.1 sawa sawa na asilimia 65 ya utekelezaji na kazi inaendelea kwa kasi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post