Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeendesha zoezi la ugawaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya maji katika eneo lake la kihuduma Mkoa wa Dar na Pwani huku mamia ya wateja wakijitokeza kupata huduma hiyo.
Akiongea na wananchi waliojitokeza kupokea vifaa vya maunganisho ya maji katika Wilaya ya Kinondoni na Ubungo, Meneja wa Mkoa kazi wa kihuduma DAWASA Makongo, Mhandisi Mkashida Kavishe ameeleza kuwa mwitikio umekuwa mkubwa kwa Wananchi na kuwahakikishia kuwa zoezi hilo ni endelevu na kila alieomba huduma ya Majisafi atapata huduma.
"Leo katika Mkoa wangu wa DAWASA Makongo tumetoa vifaa kwa wateja zaidi ya 114 ambao waliomba na kulipia huduma ya maji, kutoka mitaa ya Goba, Mbezi makabe, Mbezi Luis, Mlalakua, Makongo Juu, na Kimara Kilungule ambao tunaowahudumia na zoezi la kuwafungia litafanyika ndani ya siku chache na kuhakikisha kila Mwananchi anapata huduma”alisema Mhandisi Mkashida.
Hamza Hamduni mkazi wa mtaa wa Mlalakua kata ya Makongo meishukuru Serikali kupitia DAWASA kwa kutukumbuka na kutoa vifaa hivi ambayo vilisubiriwa kwa hamu, jambo linaloashiria sasa wanaenda kupata huduma ya majisafi na salama na kusaidia kufanya shughuli za maendeleo na kukuza uchumi.
Zoezi hili limeenda sambamba na kutoa elimu juu ya ulipaji wa malipo ya maji yaan ankara, utunzaji wa miundombinu ya maji, sheria zinazosimamia sekta ya Maji na mawasiliano rasmi ya Mamlaka kwa Wateja.