Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MIUNDOMBINU YA USAFI WA MAZINGIRA YABORESHWA SINZA "A"






Kazi ya ujenzi wa mifuniko ya chemba za Majitaka ikiendelea katika maeneo mbalimbali ya mtaa wa Sinza A chini ya usimamizi wa mafundi wa DAWASA.

Utekelezaji wa kazi hii maalum inalenga kudhibiti taka ngumu kuingia katika miundombinu ya majitaka na kupelekea uzibaji wa mara kwa mara unaosababisha uchafuzi wa Mazingira kwa majitaka kutiririka mtaani.

DAWASA inasisitiza matumizi sahihi ya miundombinu ya majitaka na kuwaasa wananchi kutotupa taka ngumu kama vile mifuko, mawe, neti, nguo na matairi katika chemba za majit aka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com