Katibu wa NEC Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndg. Rabia Abdalla Hamid, ameleeza kuwa katika kipindi cha uongozi wa nchi wa awamu ya sita, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, uhusiano wa Tanzania na nchi nyingine dunia umekua kwa kasi kubwa.
Ameongeza kuwa katika kipindi cha 2021 mpaka 2024, serikali ya CCM imeimarisha uhusiano wa kimataifa kwa kukuza biashara, uwekezaji, imeongeza ushawishi katika masuala mtambuka yanayohitaji ushirikiano wa kimataifa pamoja na kutafuta fedha kwa ajili ya kugharimia miradi ya kimkakati na kuongezeka kwa watalii.
Ndg. Rabia ameyasema hayo Julai 16, 2024, katika Chuo Cha Umoja wa Vijana wa CCM Ihemi, mkoani Iringa ikiwa ni muendelezo wa mafunzo ya kuwajengea watendaji na viongozi wa jumuiya hiyo ngazi za mikoa na wilaya zote nchi nzima.
Social Plugin