Na Mwandishi wetu, Kagera
Viongozi wa Dini wa Mkoa wa Kagera wameungana kwa pamoja kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Viongozi wa Kitaifa na Serikali kwa kuendelea kudumisha Amani, Utulivu, Upendano na Maelewano.
Ibada hiyo iliyowakutanisha viongozi wa Dini ya Kikristo na Kiislamu imefanyika leo Julai 28, 2024 katika Kanisa Anglikana Mt. Yohana Kimbugu - Muleba, Kagera iliyoambatana na Ibada ya Shukrani ya Miaka 12 ya Uchungaji wa Askofu Grayson Mutegeki Katunzi pamoja na Harambee ya Ujenzi wa Kanisa.
Akiongoza Ibada hiyo, Askofu wa Dayosisi ya Lweru Kanisa la Anglikana Tanzania, Godfrey Mbelwa amesema viongozi wa Dini na Waumini wana wajibu wa kuwaombea viongozi wa Kitaifa kwani wanafanya kazi kubwa ya kuwaletea wananchi Maendeleo.
“Tunawaombea Viongozi wetu kuanzia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bunge, Mahakama, Jeshi, Ulinzi na Usalama na wote wenye mamlaka mbalimbali katika nchi hii”- amesema Askofu Godfrey katika maombi yake.
“Serikali ya Awamu ya sita inaendelea kujenga mshikamano, umoja kwa kushirikiana na viongozi wa dini ili kuhakikisha jamii ya Watanzania inakuwa hofu ya kumuogopa Mwenyezi Mungu na kumtii”, amesisitiza Bashungwa.
Katika Harambee ya Ujenzi wa Kanisa, Waziri Bashungwa amewasilisha mchango wa Viongozi wa Serikali, jumla ya Shilingi Milioni 30 na kuahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wa Kanisa hilo ili ujenzi ukamilike kwa wakati.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma Mwassa amewaomba viongozi wa Dini kuendelea kuwasihi waumini kuwa wacha Mungu ili kuwa na hofu ya kutenda maovu kwenye jamii ikiwemo mauaji na ukatili wa kijinsia.