SERIKALI KUCHUKUA HATUA MADHUBUTI KUKABILIANA NA HOMA YA INI


Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Kuelekea siku ya Homa ya Ini,Barani Afrika kuna Watu milioni 60 wanaishi na maambukizi sugu ya Virusi vya Homa ya Ini aina B huku Watu milioni 10 wakiwa wanaishi na maambukizi sugu ya Virusi vya Homa ya Ini aina C.

Aidha hapa nchini inakadiriwa kiwango cha ushamiri wa ugonjwa wa Homa ya Ini ni asilimia 3.5 (aina B) na asilimia 1 (aina C).

Kutokana na hali hiyo,Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itandelea kuchukua hatua madhubuti za kudhibiti ugonjwa huo ikiwemo Kujumuisha huduma za homa ya ini pamoja na magonjwa ya ngono kwenye Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ugonjwa wa UKIMWI (NACP).

Hayo yamelezwa leo Julai 24,2024 Jijini hapa na Mkuu wa Programu za UKIMWI,Ngono,Ini,Malaria,Kifua Kikuu,Uelimishaji mifumo ya afya,Dkt.Catherine Joakim wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa hivi sasa mpango huo unajulikana kama NASHCoP ambao ulizindiliwa mwezi Novemba mwaka 2023.

Ameeleza kuwa lengo ni kuimarisha upatikanaji wa chanjo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kuimarisha upatikanaji wa matibabu ya homa ya ini .

"Takwimu za Shirika la Afya Duniani za mwaka 2021 zinaonyesha kuwa Duniani kuna watu wapatao milioni 296 ambao wanaishi na maambukizi sugu ya Virusi vya Homa ya Ini aina B na watu milioni 58 wanaishi na maambukizi sugu ya Virusi vya Homa ya Ini aina C, " amesema

Ameeleza kuwa mbali na mikakati mbalimbali iliyopo Serikali itaendelea kuelimisha wananchi kuhusu ugonjwa wa homa ya ini.

"Kila Mwaka tarehe 28 ya mwezi Julai, Tanzania huungana na nchi nyingine Ulimwenguni kuadhimisha Siku ya Homa ya Ini Duniani lengo ni kuongeza uelewa wa homa ya ini ambao husababisha ini kuvima na hivyo kupelekea uwezo mkubwa wa kupata ugonjwa kwenye ini au kansa ya ini, "amesema.

Licha ya hayo ameeleza kuwa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kimataifa ya Homa ya Ini yamepangwa kufanyika Sinza darajani, Uwanja wa TP, Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 25 hadi 28 Julai, 2024 kuanzia saa 02:00 asubuhi. Kilele cha maadhimisho haya kitakuwa tarehe 28 Julai,2024 ambapo Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa afya Ummy Mwalimu .

Ametaja huduma zitakazotolewa kuwa ni pamoja na kuhusiana na Virusi vya Homa ya Ini, VVU na lishe Upimaji wa maambukizi ya ini, Chanjo za homa ya Ini
Kuunganishwa na matibabu baada ya kukutwa na maambukiziUpimaji wa VVU,Upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza(kisukari na shinikizo la damu.

Pamoja na Mambo mengine kauli mbiu ya mwaka huu wa 2024 inasema "Ni Wakati wa Kuchukua Hatua" ikiyataka mataifa kuongeza kasi na juhudi makusudi katika huduma za kinga, uchunguzi na tiba ili kupunguza vifo vitokanavyo na maambuki ya virusi vinavyosababisha homa ya ini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post