TRA KUWAPANDISHA KIZIMBANI WAFANYABIASHARA 27 MOROGORO



Meneja wa TRA mkoa wa Morogoro Sylver Rutagwelera

Na Christina Cosmas, Morogoro

MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Morogoro inatarajia kuwafikisha mahakamani wafanyabiashara 27 kwa  kutozingatia matumizi ya mashine za Kielektroniki (EFD).

Meneja wa TRA mkoani hapa Sylver Rutagwelera alisema wafanyabiashara hao ni pamoja na wanaokataa kutoa risiti za EFD kwa wateja, wanaojaribu kuwatoza wanunuzi fedha za ziada ili wawapatie risiti za kielektroniki na wanaodaiwa madeni ya muda mrefu.

Rutagwelera alisema wafanyabiashara hao ni pamoja na wenye maduka ya nguo, vyombo vya ndani na bidhaa zingine ambao wamefuatiliwa kwa muda wa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2022/24 ambapo zoezi hilo ni endelevu.

Alisema tayari kesi tisa zimeshaingia katika mfumo wa mahakama na zingine zitaingizwa na kufikia 27 na kwamba 21 ni kwa ajili ya kukiuka matumizi ya EFD, kutolipa adhabu wanazopewa, wanaandikiwa barua hawajirekebishi na wengine sita (6) ni kwa ajili ya madai ya kodi za nyuma.

Alisema wafanyabiashara hao tayari walishapewa adhabu na TRA na kutakiwa kulipa kwa awamu ambapo walishindwa kufanya hivyo na kuilazimu TRA kutumia sheria zilizopo kuwafikisha mahakamani.

Hivyo aliwasihi wafanyabiashara kama walivyojitahidi kukata bima kwa ajili za biashara zao wanapaswa kutumia mashine za EFD ili ziwasaidia wakati shida zinapojitokeza ambapo alitolea mfano mvua kubwa zilizonyesa hivi karibuni na kusababisha hasara kwa baadhi ya wafanabiashara ambao wengi wao waifanyiwa maahesabu kupitia taarifa za kodi.

Naye Afisa Mwandamizi wa huduma na elimu kwa mlipakodi Immaculete Chaggu alisema watu wanavyokwepa kulpia kodi kupitia risiti za EFD ndivyo wanavyojaribu kupoteza mapato ya serikali yanayosaidia katika matumizi mbalimbali ikiwemo kuweka miradi ya maendeleo nchini.

Naye Afisa msaidizi wa kodi Abraham Mwabulambo alisisitiza matumizi ya EFD kwa wafanyabiashara ili kurahisisha ukadiriaji wa kodi ya mapato kwa maendeleo ya umma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post