Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amekutana na Rais wa Urusi, Mhe. Vladimir Putin Jijini St. Petersburg nchini Urusi leo tarehe 12 Julai, 2024 kwa lengo la mazungumzo kuhusu namna bora ya kuimarisha amani Duniani.
Dkt. Tulia
amesema Kuhusiana na mgogoro unaoendelea baina ya Urusi na Ukraine wameanza
mazungumzao na viongozi wa nchi zote mbili ili kumaliza mgogoro baina ya nchi
hizo mbili.
“Kabla ya kuzungumza naye tayari tulishazungumza na Maspika wa nchi zote hizo mbili na sisi kama Umoja wa Mabunge Duniani tumezungumza naye kama Kiongozi wa nchi katika sura ambayo tunaweza kuziweka pamoja nchi zote mbili na tutarajie kwamba IPU itatengeneza fursa ya Mabunge ya pande zote ili kuweza kuzungumzia amani katika maeneo yao ya utawala”, amesema Dkt. Tulia.
Social Plugin