UHABA WA VITABU WAKWAMISHA MATUMIZI YA MTAALA MPYA



Na Dotto Kwilasa, Dodoma

SERIKALI imehairisha matumizi ya mtaala mpya wa elimu kwa wanafunzi wa kidato tano Kwa mwaka 2024/2025 kutokana na kuchelewa kwa vitabu vinavyochapishwa kutoka nje nchi.

Imesema kuharishwa kwake kumetokana na maoni ya wadau mbalimbali wa elimu walioadhimia kuwa mtaala huo uanze kutumika mwakani.

Taarifa hiyo inakuja baada ya kuwepo kwa taarifa zinazasambaa mtandaoni kuwa serikali imesitisha kutokana na uhaba wa walimu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa. Adolf Mkenda alisema mtaala huo utaanza kutumika mwakani.

"Tumeamia kuhairisha matumizi ya mtaala mpya wa elimu kwa wanafunzi wa kidato Cha tano kutokana na uhaba wa vitabu ambavyo vinatarajia kuwasili mwisho wa mwezi huu. Hadi kuzisambaza katika shule zetu tayari muda utakuwa umeisha,"alisema

Ameongeza kuwa :" Uamuzi huo umekuja baada ya wadau wa elimu kukaa kwa pamoja na kukubaliana kuwa mtaala huo utaanza mwakani ili uende sambamba na serikali ikakubali,"

Katika hatua nyingine Profesa Mkenda alisema kwa upande wa mtaala wa wanafunzi wa awali na shule za msingi unaenda vizuri.

Amewahakishia watanzania kuwa kutokana na maono ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu yajayo yanafurahisha.

"Mitaala mingine kwa shule ya awali na msingi inaenda vizuri na niwahakikishie kuwa yajayo yanafurahisha katika sekta ya elimu kutokana na dhamira ya Rais Dk Samia ,"amesema

Kwa mujibu wa Profesa Mkenda mefafanua kuwa serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufundisha na kufundishia ili wanafunzi wanaomaliza wawe na soko Ndani na nje ya nchi.








Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post