VIWANDA VYOTE NCHINI KUFANYA KAZI


Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Selemani Jafo amesema atahakikisha viwanda vyote vilivyowekezwa Tanzania anavisimamia ili viendelee kuzalisha na kuchangia uchumi na ajira kwa Watanzania.

Dkt. Jafo ameyasema hayo Julai 08, 2024 alipotembelea Kiwanda cha Mbolea cha Itracom Fertilize Limited kilichopo Dodoma ikiwa ni baada ya kuingia ofisini kwake.

Alisema jitihada za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan zimewezesha kuongeza uwekezaji ukiwemo wa viwanda na kuwa hatahakikisha viwanda vilivyowekeza hapa nchini vinaendeleankufanya kazi kwa ufanisi.

Kuhusu kiwanda cha Itracom Fertilizer Limited, Dkt. Jafo alimuhakikishia Mwekezaji huyo kuwa atashughulikia changamoto zilizopo kwa kishirikiana na Taasisi za kisekta ili kuona kiwanda hicho kinafanya kazi kwa ufanisi na kwa faida.

Alisema hajaridhishwa na kuona kuwa katika uzalishaji unaofanywa na kiwanda kikubwa kiasi kidogo kinanunuliwa na watanzania wakati nchi zingine zinanua bidhaa ya mbolea kwa wingi.

“Kama Rais Samia amehangaika mpaka kiwanda hili kikawekezwa hapa nchini, na katika mauzo ya tani 66,000 sisi Watanzania tumenunua tani 4,238 hii haitii moyo na haifurahishi kwa kweli.”

Aidha, Dk Jafo alitumia fursa hiyo kuwahimiza Watanzania kuhakikisha wanatumia mbolea inayozalishwa hapa nchini kuliko kukimbilia zile zinazozalishwa nje ya nchi.

Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani Bw. Kimaramuziro Nkurikiye alisema uzalishaji ulianza Desemba mwaka 2022 mbolwa hiyo inafika katika mikoa 21 ambapoa hadi sasa kimezalisha tani tani 75,000 huku mbolea iliyouzwa ni tani 66,000 ambapo tani 4,238 zimeuzwa nchini, tani 52,892 zimeuzwa Kenya na tani 10,000 zimeuzwa Burundi.

Awali, Mkuu wa kitengo cha utafiti, Bw. Elias Ulyongabo alisema kwa sasa kiwanda kinatengeneza mbolea ya kupandia, kukuzia na kunenepesha na kiko katika hatua za mwisho katika kukamilisha utafiti wa mbolea kwa ajili ya mazao ya tumbaku, chai, parachichi na zabibu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post