Wananchi wameendelea kujitokeaza kwa wingi katika banda la Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kupata huduma na uelewa wa masuala mbalimbali yanayotekelezwa na ofisi hiyo.
Aidha, katika maonesho hayo Ofisi ya Waziri Mkuu inashiriki pamoja na Taasisi zake na imeendelea kuwaelimisha na kuwafahamisha wananchi na wadau juu ya masuala mbalimbali yanayotekelezwa na ofisi hiyo ikiwemo masuala ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira na Ukuzaji Ujuzi, Ustawi wa Watu wenye Ulemavu, Hifadhi ya Jamii, Uratibu wa Maafa, Uratibu wa shughuli za Serikali, Ufuatiliaji na tathmini za shughuli za Serikali, Sheria za Uchaguzi, udhibiti wa ukimwi, udhibiti wa dawa za kulevya na fursa za uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Maonesho hayo ya biashara ya kimataifa (Sabasaba) yaliyoanza Mei, 28 2024 jijini Dar es Salaam ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu inashiriki pamoja na Taasisi zake ikiwa ni sehemu ya kusogeza huduma karibu na wananchi.
Social Plugin