Na Woinde Shizza ,ARUSHA
Wananchi wamehimizwa kuachana na kilimo cha mazoea, ambacho mara nyingi kinaendeshwa kwa kutegemea hali ya hewa na mbegu za asili zisizozalisha kwa wingi ,badala yake, wanapaswa kujikita katika kilimo biashara ambacho kinahusisha matumizi ya mbegu bora, mbolea za kisasa, na teknolojia ya umwagiliaji hii itasaidia kuongeza mavuno na kuboresha maisha ya wakulima.
Kilimo biashara ni mfumo wa kilimo unaolenga kuongeza uzalishaji na faida kwa mkulima kupitia matumizi ya mbinu za kisasa na teknolojia bora.
Hayo yamebainishwa na mratibu uhaulishaji teknolojia na mahusiano kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo na mbegu TARI seliani Mosses Bayinga ambaye pia ni mratibu wa maonyesho ya kilimo biashara yanayotarajiwa kufanyika kwa muda wa siku mbili katika viwanja vya taasisi hiyo vilivyopo kisongo ndani ya halmashuri ya jiji la Arusha ambapo alibainisha kuwa wameamua kufanya maonyesho kwa ajili ya kuwapa elimu wakulima pamoja na kujifunza elimu mpya ya teknolojia mbalimbali za kilimo zinazotoka katika sekta binafsi na zaumma .
Alibainisha kuwa maonyesho hayo yanavutia zaidi ya wakulima 1000 na yatashirikisha wakulima zaidi ya 600 kutoka mikoa ya Kanda ya kaskazini ambayo ni Arusha , Kilimanjaro na manyara huku akitaja kauli mbiu ya maonyesho hayo kuwa ni tumia teknolojia bunifu za kilimo Kwa uhakika wa chakula na lishe vijana wakati ni sasa
Akitaja faida ya kwanza ya kilimo biashara ni kuongeza uzalishaji ni pamoja Kutumia mbegu bora na mbolea za kisasa huchangia kupata mavuno mengi zaidi ikilinganishwa na kilimo cha mazoea. Kwa mfano, ekari moja ya shamba la mahindi inaweza kutoa magunia 20 kwa kilimo cha mazoea, lakini kwa kilimo biashara, ekari hiyo inaweza kutoa magunia 50 au zaidi , hii ina maana kwamba mkulima atakuwa na mazao mengi ya kuuza, hivyo kuongeza kipato chake.
Alisema pia kilimo biashara huongeza thamani ya mazao Kwa kutumia teknolojia za kisasa kama vile kuhifadhi mazao kwa njia bora, wakulima wanaweza kuhakikisha kuwa mazao yao yanafika sokoni yakiwa na ubora wa juu,na hiyo inawapa nafasi ya kuuza mazao kwa bei nzuri, tofauti na kilimo cha mazoea ambapo mazao mengi huharibika kabla ya kufika sokoni kutokana na uhifadhi mbaya.
Aisha alisema kuwa kilimo biashara huchangia katika ukuaji wa uchumi wa taifa kwani Wakulima wakiwa na kipato cha juu, wataweza kutumia pesa hizo kwa mahitaji mengine kama vile elimu, afya, na huduma nyingine za kijamii na hii itachangia kupunguza umasikini na kuboresha maisha ya wananchi kwa ujumla.
Alitoa wito kwa wakulima hao kujitokeza Kwa wingi Katika maonyesho hayo ili kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo biashara na kubainisha kuwa ni wakati sasa wa wakulima kujiunga na mapinduzi ya kilimo biashara ili kujiletea maendeleo na ustawi.
Social Plugin