WAKATI watanzania wakiadhimisha siku ya Homa ya Ini Duniani imeelezwa kwamba wagonjwa wanaougua ugonjwa huo asilimia kubwa hawaoni dalili za moja kwa moja isipokuwa asilimia ndogo.
Hayo yalibainishwa leo na Daktari wa Kituo cha Siha Polyclinic cha Jijini Tanga Kasanga Bashir Kasanga wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku hiyo ambapo wameazimisha kuwa kutoa vipimo bure kwa wananchi wa mkoa huo.
Alisema kwamba dalili za awali mara nyingi zinakuwa ni zile ambazo sio za moja kwa moja “Non Specific Symptoms” ambazo zinaweza kufananishwa na magonjwa mengine na kwa dalili ambazo ni viashiria vya moja kwa moja vya homa ya ini ni hali ya manjano kwenye sehemu za macho na mabadiliko ya ngozi mikono kubadilika rangi,rangi ya choo kubadilika ,maumivu ya tumbo na kukosa hamu ya kula.
Aidha alisema kwamba athari za homa ya ini iwapo kwamba matibabu yake hayajafanyika itapelekea ini kushindwa kufanya kazi yake ya kawaida na kupelekea vifo huku akiitaka jamii kuona umuhimu wa kupata chanjo ya homa hiyo ili kuweza kukabiliana nayo.
“Ndugu zangu leo wakati tunaadhimisha siku ya homa ya Ini Duniani ni vema kutoa wito kwa wananchi kuona umuhimu wa kujitokeza kupima na iwapo wakibainika kuwepo na ugonjwa huo waanza kuchukua hatua za kukabiliana nao”Alisema
“Kwa sababu mwamko wa wananchi kujitokeza kupima unasuasua lakini ukichukua takwimu kule tulipotoka na tunapoelekea kwa kweli mwamko umeshaanza kuwa ni mzuri kwa siku ya leo mwamko umekuwa ni mzuri na hatua zinazoonekana kulingana na mwamko wa watu ni nzuri na hiyo ni kuendelea kupongeza juhudu mbalimbali ambazo zinafanywa na Wizara ya Afya na Shirika la Afya Duniani (WHO)”Alisema
Akizungumzia umuhimu wa kuchanja homa ya ini alisema kuna umuhimu mkubwa kwa sababu ya takwimu zinaonyesha kwa magonjwa makubwa ya matatizo ya homa ya ini asilimia 45 mpaka 50 yanachangiwa na homa za ini
“Hivyo umuhimu wa kuchanja ni kuhakikisha jamii inabaki salama bila kuwa na magonjwa hayo homa ya ini hepatitis B,C kutokana na kwamba hatua za mwanzo haina dalili isipikuwa dalili zinajitokeza wakati ugonjwa umekuwa umefika mbali zaidi”Alisema
“Nitumie siku hii kuwahamasisha jamii ione umuhimu wa kuchanja kwa maana iweze kujikinga na hepatitis B maana ni muhimu unapochanja Hepatitis B uweze kujua pia na Hepatitis C "Alisema
Awali akizungumza Awadhi Abdul kutoka kwenye Kituo hicho alisema kwamba wao wameamua kuadhimisha siku hiyo kwa kufanyia watu vipimo vya homa aya ini na kutoa chanjo wao kama siha wanajitahidi kuhakikisha jamii inapata uelewa katika masuala ya kiafya lakini kutoa matibabu mbalimbali kwa jamii.
Aidha alisema kwamba ukiachia na homa ya ini wao wanatoa huduma mbalimbali za kimatibabu wana madaktari bingwa, huduma za maabara na huduma za mionzi mbalimbali, CTScan na MRI kwa gharama nafuu na zinazojali hali ya mtanzania.
“Tunashukuru kwa mwitikio ambao wameupata kwa jamii na lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanapiga vita homa ya ini kwa wananchi kwa kutoa elimu “Alisema
Naye kwa upande wake Daktari Jovin Amani alisema homa ya ini inathari kwa ujumla na dalili zake ni kujisikia kuchoka na viungo kuuma,kupata manjano,kupoteza fahamu au kutapika damu.
Hivyo wanawashauri watanzania waweze kujitokeza kupima ili kujua afya zao kwa ujumla maana homa ya ini i inaweza kuambukiza mtu yoyote inaweza kusambazwa kutoka mtu moja hadi mwengine.
Social Plugin