Na Dotto Kwilasa,Dodoma
Serikali imewataka Wanufaika wa ufadhili wa Mafunzo ya muda mrefu awamu ya pili kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali wanaokwenda kusoma Ughaibuni kuwa mabalozi kwa Watumishi wengine ili kuleta tija katika kuongeza ubunifu,kueleimisha na kusukuma gurudumu la mabadiliko ya Kidijitali nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla ameeleza hayo Julai 12,2024 Jijini Dodoma katika hafla ya kutoa vyeti na kutia saini Mkataba wa kutumikia Serikali baada ya kumaliza Masomo kwa Watalaam wa Tehama waliopata ufadhili kupitia kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali.
Amesema kuwa wao kama Wizara tayari wamekamilisha masuala ya maboresho kwa kuendelea kufanyia baadhi ya mifumo ikiwa ni pamoja na kukamilisha mkakati wa miaka 10 wa uchumi wa Kidijitali unaolenga ujuzi wa jamii ya Kidijitali.
"Ujuzi mtakaopata utusaidia taaluma yenu na kuwasaidia Watumishi wenzenu kubuni,kuelimisha na kusukuma gurudumu la mabadiliko ya Kidijitali,sisi kama Wizara tumekamilisha baadhi ya masuala mbalimbali tunaendelea kuyafanya, " amesema
Mbali na hayo ameeleza kuwa kama Wizara wamekamilisha mkakati wa miaka 10 wa uchumi wa Kidijitali, unaolenga ujuzi wa jamii ya Kidijitali ambayo ni kuwa na jamii inayojua Teknolojia katika biashara na mambo mengine ya biashara mtandao.
Kutokana na hayo Salvatory Mbilinyi ambaye ni Mkurugenzi Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ameewaasa wanufaika hao kutokubeza tamaduni za watu pale watakapokwenda masomoni hasa tamaduni za mavazi japo inategema na nchini husika,ili kutojiingiza katika malumbano yasiyo ya lazima.
"Sisi Watanzania tuna tamaduni tofauti na wenzetu msiende kubeza tamaduni za watu,mfano katika mavazi maana unaweza kukutana na mtu kavaa ambavyo huwezi kuelewa usioneshe kuchukizwa na Utamaduni wake,we muangalie kama alivyo kwasababu anaweza kuchukia pia,lakini hiyo inategemea umeenda nchi gani".
Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi na utawala bora Ibrahim Mahumi amewataka wakafuate Sheria,Taratibu na Kanuni na kuongeza kuwa ni mategemeo ya Ofisi ya Raisi na Utumishi na Serikali kwa ujumla kuwa wanufaika hao watakapo kwenda masomoni watafanya kile ambacho kinakusudiwa kufanyika na sio Mambo mengine.
Akitoa Shukurani kwa niaba ya wanufaika wote Mhandisi Mwandamizi kutoka mfuko wa mawasiliano kwa wote Brian Kasuma amesema kuwa watatumia fursa hii adhimu kwa kujibiidisha katika masomo ili kuweza kuchangia katika maendeleo ya nchi na hasa katika uchumi wa Kidijitali na kuahidi kuwa mabalozi wa kuitangaza Tanna vivutuo vyake.
"Tunaahidi kutumikia vyema fursa hii adhimu kwa kujibidiisha katika masomo ili kuweza kuchangia katika maendeleo ya nchi yetu hasa katika uchumi wa Kidijitali. Pia tunaahidi kuwa wazalenndo wa nchi yetu na mabalozi wazuri wa jamii ya nchi yetu kwa kutii sheria na taratibu nchi husika tunazoenda kusoma na kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii kila tutakapopata nafasi".
Pamoja na mambo mengine Wanufaika waliosaini Mkataba huo na kupokea vyeti kwa ni 30 ambapo ni awamu ya pili na awamu ya kwanza walikuwa 20 hivyo jumla wamefikia 50 ambapo ndio idadi iliyokuwa ikihitajika.