Waziri wa maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amekutana na kuzungumza na watumishi wa Mikoa kazi DAWASA Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Tegeta, Mivumoni, Kawe pamoja na watumishi katika mitambo ya kuzalisha maji Ruvu juu na chini na kuwataka kufanya kazi kwa bidii na kuipenda kazi yao.
Waziri Aweso amesisitiza kuwa pamoja na kazi kubwa inayofanyika bado ni muhimu Kuongeza juhudi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji na kuhudumiwa kwa weledi mkubwa.
Kwa upande wao watumishi hao wamemuahidi Waziri wa Maji kubadilika na kufanya kazi kwa kujituma zaidi huku wakitambu umuhimu wa huduma wanayoitoa Kwa jamii.
Mhe. Jumaa Aweso Waziri wa Maji yupo katika muendelezo wa ziara yake katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam DAWASA yenye lengo la kukagua na kuboresha utendaji kazi wa Mamlaka.
Social Plugin