Na Oscar Assenga, TANGA
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema hatarajii kuona fedha zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya hati fungani zinadokolewa au kuchezewa badala yake wahakikishe zinatumika kwenye malengo yaliyokusudiwa na kurejeshwa kwa utaratibu waliojiwekea.
Aweso aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa halfa ya utiaji
saini ya mikataba utekelezaji wa miradi ya maji kwa fedha za hati fungani kati
ya Tanga Uwasa na Wakandarasi STC Contracstion Limited na China Railway 7 Group
Limited katika halfa iliyofanyika kwenye ofisi za Mamlaka hiyo
Alisema kwamb wanapaswa kuhakikisha wanazilipa ili wapate nguvu
na maeneo mengine waweze kufaidika na huo ndio uelekeo wa Serikali kwa mamlaka
za maji nchini.
Alisema kwamba jambo ambalo limefanywa na mamlaka hiyo ni kubwa
huku akimuangiza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Agnes Meena kumfikisha
salamu katibu Mkuu lazima utendaji wake na usimamizi katika mradi huo pamoja na
ufuatiliaji uwe wa kipekee ili kufanikisha dira na dhamira ya Rais Dkt Samia
Suluhu.
“Tunapozungumza fedha za wananchi wameweza katika hati fungani
na mwananchi namba moja aliyetoa fedha kwa ajili ya kusapoti maji katika Jiji
la Tanga ni Rais Dkt Samia Suluhu hivyo niwasihi tusidokee na tusichezee huu
mradi tuende kutumiza malengo ya Rais “Alisema Waziri Aweso
Hata hivyo aliwataka wakandarasi ambao wamepata dhamana ya kutekeleza
mradi huo wao kama Wizara jicho lao litakuweo hapo muda wote kusimamia na kufuatilia hivyo wanahitaji kuona tija
kubwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.
“Bodi ya Tanga Uwasa tunapozungumzia hati fungani ni fedha za
wananchi wamesema hivyo fedha kama wamekopeshwa lazima kuzirejesha na faida wasije wakawa watu wa maneno
hawataeleka ile nia njema nzuri ambayo waliopanga kuifanya itabadilisha taswira
ya Taasisi yenu…niwapongeze Tanga Uwasa ukiwa baba au mzazi ukiona mtoto wako
anafanya kazi nzuri jukumu lao ni kumuombe dua hivyo mimi ninawaombe
dua”Alisema
Awali akizungumza wakati wa halfa hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo
alisema kwamba wameingia kwenye historia katika miradi waliosaini hapo
wanakwenda kuitekekeza ni sehemu ya mradi mkubwa wa hati fungani kama alivyoeleza
Waziri kinachotokea ni wananchi kuwekeza kwenye huduma ya maji.
Alisema fedha zao zinaende kutoa huduma ya maji na hivyo baadae
kupata faida jambo hilo ni la kwanza kufanyika hapa nchini kupitia mamlaka hiyo
huku akimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu wazo
hilo lilipofika kwake aliona ni njia nzuri ya kusaidia serikali kugharamia
miradi ambayo serikali inapata ugumu kuigharami kwa sababu ya uwepo wa miradi
mingine mikubwa ya kipaumbele .
“Hivyo akikubaliana na wazo hilo litekelezwe na amekuwa pamoja
nasi muda wote mpaka sasa na Rais amewekeza ni moja ya watu waliowekeza kwenye
hati fungani na wengine ambao wamewekeza ambao wamejitokeza na kukudhi kwa muda
mfupi kupata kiasi cha zaidi ya Sh.Bilioni 53 walichokuwa wakikihitaji lakini
kimevuka lengo mpaka Bilioni 54 “Alisema Mkurugenzi huyo wa Bodi ya
Wakurugenzi.
“Niwashukuru wawekezaji ambao wamewekeza kwenye hati fungani
niwaambie fedha zenu sipo salama na hazitapotea na hakuna hata moja na
zitafanya kazi iliyokusudiwa na tumejipanga kufanya mradi huo na Mhe Waziri
usiwe na wasiwasi ikifika wakati wa kulipana faida na tutaanza na mwezi Octoba
mwaka huu na Aprili mwakani kila mwaka na wamejipanga kutekeleza hilo” Alisema
Naye kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Agnes
Meena akizunguma katika halfa hiyo alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa
kuendelela kuipa kipaumbele cha hali ya juu sekta ya maji na hivyo kuwawezesha kuendelea
kutekeleza majukumu yao kwa wepesi.
Naye kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Gilbert alisema kwamba mkoa huo umeendelea kuimarisha
hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira kwa wananchi
ambapo miradi mbalimbali ya kimkakati inaendelea kukamilika na kuwezesha
upatikanaji wa huduma bora
“Tunaishukuru Serikali kwa kuendelea kuipa nguvu sekta ya Maji
kwa mkoa wa Tanga jumla ya miradi 67 yenye thamani ya Bilioni 89.67
inatekelezwa kupitia Ruwasa na miradi 13 yenye thamani ya Bilioni 11.32 inatekelezwa
na Tanga Uwasa hivyo tunaendelea kuishukuru serikali kwa kuendelea kupambania
wananchi wa mkoa huu na kuendelea kuimarisha shughuli za kijamii na kichumi”Alisema