Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI BASHE KUFUNGUA MKUTANO WA 27 WA BENKI YA KCBL DODOMA


Mwenyekiti wa Benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (KCBL) Prof.Gervas Machimu akizungumza na Waandishi wa habari leo Julai 25 Jijini Dodoma kuhusu Mkutano Mkuu wa 27 wa Benki hiyo unaitarajiwa kuanza Julai 26 mwaka huu.

Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Waziri wa Kilimo nchini Husein Bashe anatarajiwa kufungua mkutano wa 27 wa Wanahisa wa benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (KCBL) na wanahisa wengine walionunua hisa katika benki hiyo ili kufanya tathimini ya utendaji kazi wake.

Mwenyekiti wa Benki hiyo Prof.Gervas Machimu ameeleza hayo leo Julai 25,2024 Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa habari huku akiwataka wanahisa hao kufika Mkutano huo mkuu wa 27 utakaofanyika jijini Dodoma Julai 26 2024 .

Prof. Machimu amesema lengo kuu la mkutano huo ni kwenda kueleza na kuwapa majibu wanahisa kwa yale yote walioagizwa ikiwa ni pamoja na kueleza matarajia ya mwaka ujao.

"Mkutano huo utakaofanyika jijini kesho Julai 26,2024,mkutano huo unafanyika kwa Mara ya kwanza Dodoma na ni wakihistoria kwani ni wa mwisho wa benki ya KCBL na sasa tunakwenda kuanzisha benki ya Ushirika ya kitaifa ambayo inauganisha benki mbili KCBL na benki iliyokuwepo, "amefafanua

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa KCBL Godfrey Ng'urah amesema mkuano huo unahusisha wanahisa wote wa Benki hiyo na kuwa baada ya miaka mitatu yamchakato wa mageuzi wanaushirika watafanya mkutano wao kwa mara ya kwanza .

"Ajenda mahususi ni pamoja na utendaji kazi wa mwaka jana 2023 uliokuwa na mafanikio makubwa katika utendaji lakini pia mkutano huu utaonyesha safari yetu ijayo ya miaka 3 ya mageuzi kama walivyotuagiza kwenye mkutano Mkuu wa mwaka uliopita na kuipa bodi mamlaka ya kukamilisha safari hiyo ya mageuzi kuwa Benki ya ushirika Tanzania, "amesema.

Meneja huyo ameeleza kuwa,"kupitia benki hii Wanahisa wanayo fursa ya kupata matokeo ya kazi kubwa iliofanywa na bodi kwa kushiriana na Menejimeti .

" Imani yetu ni kuifanya benki ya Ushirika ya Kilimanjaro kuwa benki moja ya Ushirika Tanzania, pili kuwa na matokeo ya kiutendaji na Shughuli mbalimbali za kibiashara, bidhaa, huduma za kifedha huko tumefanikiwa kwa kipindi cha miaka mitatu, "anasisitiza Ng'urah.

Sambamba na hayo amezungumzia uendeshaji wa mifumo utawala bora kuwa na usimamizi wenye tija uliotokana na Shughuli na uongozi wa 2023 na wanahisa kupitisha maazimio mbalimbali ikiwemo hatua za mwisho za kurasimisha Benki ya Ushirika Tanzania.

Amefafanua kuwa moja ya maazimio makubwa Katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2021 hadi 2023 ni kuhamisha makao makuu kutoka Kilimanjaro kuja Dodoma huku amesisitiza kuwa hadi kufikia September 9 mwaka huu kila kitu kitakuwa sawa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com