Wenyeviti wa mitaa ,vijiji na vitongoji Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wamefanya sherehe ya kujipongeza kwa utendaji kazi wao wa miaka mitano.
Sherehe hiyo imefanyika katika ukumbi wa chuo cha walimu Shinyanga ikiambatana na zoezi la kuchangia damu katika benki ya damu iliyopo katika hospitali ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga kwa lengo la kusaidia makundi ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu wakiwemo wajawazito,watoto na waathirika wa ajali.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika Sherehe hiyo Anord Makombe ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini amewataka wenyeviti hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii ya kuwahudumia wananchi katika kipindi hiki ambacho wanajiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa.
Naye mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu Moke warioba ambaye pia ni mwenyekiti wa wenyeviti wa serikali za mtaa Manispaa ya Shinyanga amewashukuru wenyeviti kwa ushirikiano wao ambao wanaendelea kumpatia na kuomba ushirikiano huo uendelee wakati wanapoendelea kuwatumikia na kutatua kero za wananchi.
Social Plugin