Na Marco Maduhu,KISHAPU
WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde ametembelea katika Mgodi wa Almasi Mwadui (WDL) uliopo Wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga na kukumbana na changamoto mbalimbali ikiwamo kushuka kwa soko la Almasi duniani.
Amefanya ziara hiyo leo Agosti 19,2024 akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa wizara hiyo, pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge nishati na madini.
Amesema changamoto ya kushuka kwa soko la madini ya Almasi ni ya dunia nzima siyo Mwadui pekee,hivyo Serikali itaendelea kushirikiana na Mgodi wa Almasi Mwadui katika utatuzi wa changamoto hiyo ili kurudisha heshima na hadhi ya madini ya Almasi.
"Changamoto hii ya kushuka kwa soko la madini ya Almasi zipo sababu kuu 4,moja ikiwa ni kuwapo kwa uzalishaji wa madini ya Almasi za Maabara ambazo bei zake za chini," amesema Mavunde.
"Kushuka kwa soko hili la Almasi hata sisi Serikali ambao tuna ubia na mgodi huu tutakosa mapato, na tuta hakikisha tunashirikiana na mgodi kuitatua ili kurudisha heshima na hadhi ya madini ya Almasi," ameongeza Mavunde.
Aidha,ametoa maagizo kwa Mgodi kwamba kwa wale watoa huduma ndani ya mgodi huo(Local Content) wakae nao na kuwaeleza hali halisi ya kushuka kwa soko la Almasi na siyo kuwapunguza bila kuwapatia taarifa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,amesema Serikali ya Mkoa huo wataendelea kushirikiana na wawekezaji, huku akisisitiza suala la uzalendo hasa kwenye ulipaji wa mapato ya serikali.
Amesisitiza pia suala la uimara wa mabwawa ya kuhifadhia majitope yawe imara na kufanyiwa ukakuzi wa mara kwa mara, ili kusije tokea tena madhara ya kupasuka kwa bwawa katika mgodi huo.
Meneja wa Mgodi wa Almasi Mwadui Ayoub Mwenda awali akisoma taarifa ya uzalishaji wa mgodi huo, amesema umeongezeka lakini wanakabiliwa na changamoto moja kubwa ya kushuka kwa soko la Almasi duniani.
Amesema kushuka kwa soko hilo kumesabisha kupata mauzo hafifu ya Almasi licha ya kuwa na uzalishaji mkubwa, huku wakianza kupunguza matumizi ambayo siyo ya lazima pamoja na watoa huduma ndani ya mgodi huo.
Aidha, amesema mikakati waliyonayo kama mgodi ni kuongeza ukubwa wa Almasi ambayo wataizalisha, pamoja na kuiongezea thamani na ubora zaidi ili kuzizidi Almasi za kwenye maabara.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Nishati na Madini Masache Kasaka,ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kukuza sekta ya madini hapa nchini.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Waziri wa madini Anthony Mavunde (wapili kutoka kulia) akiwa katika Mgodi wa Almasi Mwadui, (kulia) ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge Nishati na Madini Masache Kasaka, (kushoto)ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.
Waziri wa Madini Anthony Mavunde akiwa katika Mgodi wa Almasi Mwadui.
Waziri wa Madini Anthony Mavunde akiwa katika Mgodi wa Almasi Mwadui.
Waziri wa Madini Anthony Mavunde akiwa katika Mgodi wa Almasi Mwadui.
Waziri wa Madini Anthony Mavunde akiwa katika Mgodi wa Almasi Mwadui akiagana na viongozi mara baada ya kumaliza ziara yake.
Waziri wa Madini Anthony Mavunde akiwa katika Mgodi wa Almasi Mwadui akiagana na viongozi mara baada ya kumaliza ziara yake.
Social Plugin