Mgeni rasmi, Naibu Mkuu wa Mafunzo Taasisi ya Elimu ya Watu wazima Bi. Marry Watugulu akinunua mazao ya wakulima wa mbogamboga
Kikundi cha akina mama wanaolima bustani za mbogamboga jijini Dar es salaam kinachojulikana kwa jina la 'Mwanamke Bustani' kimeadhimisha Sikukuu ya Wakulima Nane Nane kwa kuendesha semina za mafunzo kwa vitendo kuhusu masuala ya ujasiriamali, elimu ya pesa kutoka Benki ya NMB , uwekezaji kutoka U.T.T AMIS ,elimu ya malezi na makuzi kwa watoto.
Mgeni rasmi katika mafunzo hayo yaliyoongozwa na kauli mbiu isemayo 'Mwezeshe Mwanamke kwa ustawi wa malezi bora na uchumi' alikuwa Mkuu wa Mafunzo Dkt. Marry Watugulu huku yakihudhuriwa na wadau mbalimbali wa kilimo.
Mwenyekiti na mlezi wa kikundi cha Mwanamke Bustani Bi. Regina Michael anayesoma Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima akichukua Shahada ya elimu ya watu wazima na maendeleo ya jamii ameeleza changamoto walizonazo kuwa ni pamoja na mtaji wa kununua pembejeo, masoko ya mbogamboga.
Amemuomba Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kusikia kilio chao ili wawezeshwe mitaji ili waweze kutimiza malengo huku wakimuomba kukutana na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe lakini pia wakiwaomba wadau mbalimbali wawafikie ili waweze kuwawezesha.