Picha : KONGAMANO LA WADAU WA MADINI....MAVUNDE AZITAKA BENKI KUIUNGA MKONO BENKI YA CRDB KUWAKOPESHA WACHIMBA MADINI

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony (mwenye tai nyekundu kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Bilioni 10 kwa baadhi ya wachimbaji wa Kanda ya Ziwa itakayotumika kuimarisha shughuli zao kwenye maeneo tofauti wanakotoka. Picha na Kadama Malunde

******
* Benki ya CRDB Yaanzisha kitengo maalum cha madini
 
*Yamwaga Mabilioni ya Fedha kuwakopesha Wachimbaji

*Tayari wachimbaji wadogo wamelamba bilioni 19

*Waziri Mavunde Aipongeza CRDB kwa kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wachimbaji
 
Na Mwandishi wetu -  Kahama

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde ameipongeza Benki ya CRDB kwa kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wachimbaji wakiwamo wadogo na kuyataka mabenki na taasisi nyingine za fedha kuiga mfano huo.

Mheshimiwa Waziri Mavunde ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Agosti 19,2024 mjini Kahama alipokabidhiwa ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa utoaji huduma za fedha kwa wachimbaji wadogo na wa kati kutokana na maelekezo aliyoyatoa mwaka 2023 alipokutana na Wachimbaji wa madini, viongozi wa serikali, wafanyakazi wa Benki ya CRDB na wadau mbalimbali wa sekta ya madini.

Katika hafla hiyo Mheshimiwa Waziri Mavunde pia amekabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Bilioni 10 kwa baadhi ya wachimbaji wa Kanda ya Ziwa itakayotumika kuimarisha shughuli zao kwenye maeneo tofauti wanakotoka.

“Wachimbaji wadogo ni jeshi kubwa kwenye sekta ya madini nchini lakini lenye changamoto ya mtaji. Iwapo benki zetu za ndani zitawapa kipaumbele watu hawa kama mnavyofanya Benki ya CRDB, mchango wa sekta ya madini kwenye pato letu la taifa utaongezeka kwa kiasi kikubwa. Nawapongeza Benki ya CRDB kwa kuuona umuhimu wa kuizingatia sekta hii,” amesema Mheshimiwa Waziri Mavunde.
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo.

"Leo nasimama hapa kwa furaha kubwa kuwashukuru na kuipongeza Benki ya CRDB kuwa kati ya benki chache za mfano ambazo zimeamua kuja kuwawezesha na kuwainua wachimbaji, watoa huduma. Nataka niwaambie CRDB hamjapoteza, mmeingia kwenye njia sahihi. Hili eneo mlilisahau,wachimbaji wenyewe wanakopeshana, hivyo naomba taasisi za kifedha zitambue kuwa wachimbaji wanakopesheka, wana uwezo wa kulipa na mtayaona mafanikio ndani ya muda mfupi kupitia hii sekta ya madini.

CRDB niwapongeze sana, kiasi shilingi Bilioni 64 mlichotoa kwa wachimbaji wa madini siyo kiasi kidogo, kinakwenda kuchochea uchumi wa sekta ya madini, kinakwenda kubadilisha maisha ya wachimbaji wadogo nchini. Hii ni nyenzo ya kuchochea sekta ya madini, CRDB hamjapotea mumewekeza sehemu sahihi na nitoe rai kwa taasisi zingine za kifedha na benki zingine kuiamini sekta ya madini",amesema Mavunde.

Mwaka jana, Mheshimiwa Waziri Mavunde aliwaeleza watendaji wa benki nchini juu ya changamoto ya upatikanaji wa huduma za fedha ikiwamo mikopo kwa wachimbaji wadogo na kuwataka kuangalia namna ya kurahisisha upatikanaji wake ili kukuza mchango wa sekta ya madini nchini ambayo inaajiri maelfu ya wananchi katika mikoa mbalimbali nchini.
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde.

Kwenye hafla hii, Mhe. Waziri Mavunde amesema Serikali itandelea kuimarisha mazingira ya uchimbaji nchini ikiwemo kujenga uwezo wa wachimbaji wadogo kufanya utafiti utakaowasaidia kuchimba maeneo yenye uhakika wa kupaa madini tofauti na hali ilivyo sasa wanapochimba kwa kubahatisha.

Mhe. Mavunde amesema Serikali inaendelea na juhudi za kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa kutekeleza mikakati tofauti kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kuwa inatambua kuwa bado wachimbaji wadogo wengi wanafanya shughuli zao bila kufanya utafiti wa kisayansi hivyo kutokuwa na uhakika wa kupata madini wanayoyakusudia.

Waziri Mavunde amesema hayo baada ya Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa kumjulisha kuhusu hatua kadhaa zilizofanywa na benki katika kuwawezesha wachimbaji wadogo pamoja na changamoto ilizokutana nazo.

Akiainisha mchango wa Benki ya CRDB, Raballa amesema imeanzisha kitengo maalum cha madini ili kutoa wigo mpana wa utekelezaji wa mikakati inayoelekezwa kwenye sekta ya madini na kujenga uwezo kwa wafanyakazi kuchambua maombi na mahitaji ya wachimbaji wadogo wa madini.

Kitengo hiki, Raballa amesema kinasaidia kuratibu utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa wachimbaji wadogo ambayo wanaipata kwa wakati unaostahili, benki inawapa huduma za bima, inafadhili ununuzi na uingizaji wa kemikali pamoja na mitambo muhimu ya uchakataji na uchenjuaji madini nchini na inawasaidia kubadili fedha za kigeni kila inapohitajika.
Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa.

“Benki yetu imeendelea kuwa mstari wa mbele kufanikisha upatikanaji wa fedha za uwekezaji wa miradi ya madini kuanzia kwa wachimbaji wadogo mpaka wakubwa. Hadi sasa tumeshakopesha zaidi ya shilingi bilioni 64. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 19 zimetolewa kwa wachimbaji wadogo,” amesema Raballa.

Kwa wachimbaji wakubwa, afisa huyo amesema Benki ya CRDB imeidhinisha mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni 120 kwenye mradi wa uchimbaji wa madini ya kinywe unaotekelezwa na kampuni ya Faru Graphite na imeteuliwa kuongoza jopo la mabenki kutafuta fedha za ujenzi wa mradi uchimbaji wa madini ya urani utakaogharimu dola milioni 900 za Marekani baada ya kuthibitishwa na Tume ya Madini.

“Benki yetu pia imeanzisha kitengo maalumu kinachosimamia mnyororo wa thamani ambacho moja ya majukumu yake ni kuwaunganisha watu na fursa zilizopo kwa kuhakikisha kinaboresha mahusiano na huduma zetu kuwafikia hadi wateja kwa wakati sahihi. Hata hivyo, kati ya changamoto kubwa zilizopo ni wachimbaji wadogo kutotunza kumbukumbu za uzalishaji na mauzo ya madini jambo linaloweza kuwaongezea vigezo vya kupata mikopo kwa urahisi,” amesema Raballa.
Wadau wa Sekta ya Madini wakiwa kwenye kikao

Naye Mkuu wa  Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha amesema mkoa wa Shinyanga ni moja ya mikoa ya kimadini ambao unatambua mchango wa sekta ya madini ambapo katika mwaka wa 2023/2024 ulifikisha asilimia 85 ya ukusanyaji wa maduhuli hivyo upatikanaji wa mikopo kwa wachimbaji wadogo utachochea shughuli za uchimbaji wa madini ambao utasaidia kuongezeka kwa mapato ya serikali.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Masache Kasaka ameipongeza Wizara ya Madini na taasisi zake kwa juhudi mbalimbali inazofanya katika mageuzi makubwa ndani ya sekta ya madini ikiwa ni sehemu ya maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Kamati ikiwemo hilo la kusimamia upatikanaji wa mikopo kwa wachimbaji wadogo.

Rais wa FEMATA John Wambura Bina

Akitoa salamu, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimba Madini Tanzania (FEMATA)  ,John Wambura Bina amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Madini ambao umeanza kuleta tija na kuaminika kwa wachimbaji wadogo kukopesheka kwakuwa sasa kuna mashine za uchorongaji zinazosaidia kupata taarifa za awali za uwepo wa madini na hivyo kuwatoa wachumbaji kwenye kuchimba kwa kubahatisha.

Kuhusu Benki ya CRDB

Benki ya CRDB ni moja benki zinazoongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki, inatoa huduma kwa wateja wadogo, wakati na wakubwa ikiwamo huduma kwa wateja binafsi, huduma za hazina, huduma za bima, mikopo ya biashara, kilimo na uwezeshaji kwa wajasiriamali wadogo.

Benki ya CRDB ndio benki ya kwanza nchini Tanzania kutambuliwa na kampuni ya kimataifa ya utafiti ya Moody’s Investors Service kuwa moja kati ya benki 10 imara na salama Afrika katika uwekezaji. Moody’s imeipa Benki ya CRDB daraja la uimara la B1 ambapo ni daraja la juu zaidi kupatikana kwa mabenki na taasisi za fedha katika ukanda wa jangwa la Sahara. Benki ya CRDB imepata utambuzi wa Mfuko wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UN Green Climate Fund) tangu mwaka 2019 na pia imetambuliwa kama benki bora Tanzania na jarida la Global Finance kwa mwaka 2020 na mwaka 2022 ilitambuliwa kama benki bora Tanzania na jarida la Euromoney.

Benki ya CRDB imekuwa kiungo muhimu cha biashara katika nchi za Tanzania, Burundi na DRC kwa kuwahudumia wateja zaidi ya milioni 4 na kupitia mtandao mpana wa matawi zaidi ya 260, zaidi ya CRDB Wakala 25,000, 550 ATM, mashine za manunuzi 1,800 na Kituo cha Huduma kwa Wateja kinachotoa huduma saa 24/7.
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga

Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akielezea hatua kadhaa zilizofanywa na benki katika kuwawezesha wachimbaji wadogo pamoja na changamoto ilizokutana nazo.

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony (mwenye tai nyekundu kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Bilioni 10 kwa baadhi ya wachimbaji wa Kanda ya Ziwa itakayotumika kuimarisha shughuli zao kwenye maeneo tofauti wanakotoka.

Msanii Magambo Machimu Lenga akitoa burudani
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini nchini (FEMATA), John Bina akizungumzawakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akitoa salamu wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akitoa salamu wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini Mhe. Masanche Kasaka akizungumzawakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Nyang'wale Mhe. Hussein Kassu akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Kamishna wa Madini nchini, Dkt. Abdulrahman Mwanga akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Meneja Mwandamizi wa Dawati Maalumu la Madini la Benki ya CRDB, Abdulrahim Msonde akizungumza wakati wa kikao hicho
 Meneja Mwandamizi wa Wateja Wadogo na wa kati wa Benki ya CRDB, Agness Kisinini akitoa akizungumza kwenye kikao hicho

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (mwenye suti ya bluu) akiangalia kikundi cha burudani ya ngoma ya utamaduni ya Kabila la Wasukuma
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (mwenye suti ya bluu) akiangalia kikundi cha burudani ya ngoma ya utamaduni ya Kabila la Wasukuma
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (mwenye suti ya bluu) akitoa zawadi kwa kikundi cha burudani ya ngoma ya utamaduni ya Kabila la Wasukuma
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (kushoto),Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa 
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (kushoto), akisaimiana na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.

Picha za Kumbukumbu 

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Tazama Video Msanii Magambo Machimu Akitoa Burudani

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post