Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akionesha Gari aina ya TOYOTA HIACE yenye namba za usajili T. 886 DCU lililokamatwa na dawa za kulevya aina ya mirungi
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limemkamata mtuhumiwa mmoja pamoja na Gari aina ya TOYOTA HIACE yenye namba za usajili T. 886 DCU akiwa na dawa za kulevya aina ya Mirungi bunda 02 zenye uzito wa gramu 400.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Agosti 21,2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa kufuatia misako pamoja na doria zilizofanywa na Jeshi la Polisi kuanzia Julai 25, 2024 katika maeneo ya Nyakato, Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.
"Tulipata taarifa fiche kwamba Gari aina ya TOYOTA HIACE inayofanya safari zake Shinyanga - Kahama inasafirisha dawa za kulevya za kulevya, tukaweka mitego, tumekuta Mirungi bunda 02 zenye uzito wa gramu 400, mtuhumiwapia tumemkamata. Tunatoa Onyo kwa wanaofanya biashara ya dawa za kulevya, wanaosafirisha dawa za kulevya waache kwani taarifa tunazo, naomba wananchi tuendelee kupeana taarifa za uhalifu na wahalifu",amesema Kamanda Magomi.
Amesema katika msako na doria hizo pia walikamatwa watuhumiwa wawili wakiwa na madini aina ya dhahabu vipande 03 vilivyochomwa, vyenye uzito wa gramu 13.35 na mzani 01 pamoja na pesa Tsh.2,799,000/=.
"Pia Agosti 1, 2024 katika Kata ya Nyasubi, Manispaa ya Kahama, walikamatwa watuhumiwa wanne wakiwa na madini yadhaniwayo kuwa dhahabu vipande 11 vyenye uzito wa gramu 652.6, gari aina ya SUZUKI VITARA, pamoja na pesa Tsh.96,000,000/= na watuhumiwa wamefikishwa mahakamani",ameeleza Kamanda Magomi.
Vitu vingine vilivyokamatwa ni Pikipiki 06, nondo vipande 12, simu 04, kaboni mifuko 02, Godoro 02, Redio 03, jiko la gesi 01, pipa 01 la kuchenjulia dhahabu na Ving'amuzi 02.
"Jumla ya kesi 20 zimepata mafanikio mahakamani, ambapo kesi 01 ya mauaji kesi 04 kubaka washtakiwa 02 walihukumiwa kunyongwa hadi kufa, washtakiwa 04 walihukumiwa kifungo miaka 30 jela, kesi 01 ya kujiwasilisha (impersonation) mshtakiwa 01 alihukumiwa kifungo miaka 18 jela, kesi 03 kujeruhi washtakiwa 05 walihukumiwa kifungo miaka 05 jela, kesi 01 kuharibu mali washtakiwa 02 walihukumiwa kifungo miaka 03 jela, kesi 02 ajali kugonga watembea kwa miguu na kusababisha majeruhi washtakiwa 02 walihukumiwa kifungo miaka 02 jela",ameongeza Kamanda Magomi.
"Mafanikio mengine ya kesi ni kesi 03 za wizi washtakiwa 03 walihukumiwa kifungo miezi mitano jela, kesi 01 kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu mshtakiwa 01 alihukumiwa kifungo miezi minne jela, kesi 01 shambulio la kudhuru mwili mshtakiwa 01 alihukumiwa kifungo miezi 03 jela na kesi 03 kuingia kwa jinai washtakiwa 03 walihukumiwa kifungo miezi 03 jela",amesema.
Aidha amebainisha kuwa Polisi Mkoa wa Shinyanga kupitia kikosi cha Usalama barabarani wamefanikiwa kukamata jumla ya makosa 3,084 ambapo makosa ya magari ni 2,082 na makosa ya bajaji na pikipiki ni 1,002 wahusika waliwajibishwa kwa kulipa faini za papo kwa hapo, pia Madereva 02 wamefungiwa leseni ya udereva kwa kipindi cha miezi mitatu kwa kosa la kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya watu watatu.
Kuhusu utoaji wa elimu ,Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kufanya jumla ya mikutano 84 ya uelimishaji kwa jamii ambapo jumla ya vikundi 41 vya ulinzi shirikishi vimepewa mbinu za kudhibiti matukio ya uhalifu pamoja na elimu ya ukamataji salama.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Agosti 21,2024- Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Agosti 21,2024
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akionesha dawa za kulevya aina ya mirungi zilizokamatwa kwenye Gari aina ya TOYOTA HIACE yenye namba za usajili T. 886 DCU
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akionesha Gari aina ya TOYOTA HIACE yenye namba za usajili T. 886 DCU lililokamatwa na dawa za kulevya aina ya mirungi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akionesha Gari aina ya TOYOTA HIACE yenye namba za usajili T. 886 DCU lililokamatwa na dawa za kulevya aina ya mirungi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akionesha Gari aina ya TOYOTA HIACE yenye namba za usajili T. 886 DCU lililokamatwa na dawa za kulevya aina ya mirungi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akionesha pikipiki zilizokamatwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akionesha kaboni mifuko 02
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akionesha magodoro yaliyokamatwa
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin