EPZA YAHAMASISHA WAWEKEZAJI WA NDANI KUTUMIA FURSA WALIZONAZO



Na; HUGHES DUGILO, DODOMA

Serikali kupitia Mamlaka ya Uwekezaji EPZA imeendeleza jitihada zake za kuhakikisha wawekezaji wazawa wanapata fursa ya kuzalisha bidhaa zinazokidhi soko la nje ili kuiongezea nchi pesa za kigeni.

Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa uhamasishaji wa EPZA BI. Nakadongo Phares, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane-nane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

'Tuko hapa Nane-nane kutoa elimu kwa wananchi, lakini pia kuelezea fursa zilizopo za kupata maeneo maalum katika fursa za uwekezaji wa viwanda vinavyozalisha kupeleka nje ya nchi' amesema Bi. Nakadongo.

Amesema kuwa EPZA ina programu ya kumuwezesha mwekezaji kupata leseni itakayopelekea kupata eneo maalum nakuanza ujenzi wa kiwanda lengo likiwa ni kuuza nje kwa asilimia 80 na ndani asilimia 20.

Aidha Mwekezaji hajazuiliwa kufanya mauzo nje kwa asilimia 100

Pia, amefafanua kuwa Leseni anayoipata mwekezaji inamuwezesha kupatiwa eeneo maalum lililoboreshwa tayari kwa uwekezaji.

Maeneo hayo yapo Bagamoyo Pwani, Manyara, Mtwara na Tanga, pamoja na sehemu nyinge nchini, atapatiwa ili kuanza ujenzi wa kiwanda chake.

'Kwahiyo ninawahamasisha wawekezaji wetu wa ndani kuweza kutumia fursa hizi kwenye maeneo yetu maalum ya uwekezaji wa viwanda. Tusiache hii fursa ikatumiwa na watu wa nje' amesema Bi. Nakadongo.

Malengo ya kisera ya uanzishwaji wa programu ya EPZ na SEZ yaliyoanishwa kwenye kifungu cha 4 cha Sheria ya EPZ, Sura 373 na kifungu cha 5 cha Sheria ya SEZ, Sura 420 ni pamoja na Kujenga uwezo wa sekta ya viwanda kuzalisha ushindani wa masoko kibiashara ndani na nje ya Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post