Viongozi wa Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandaoni Zanzibar (ZONA) leo wametembelea ofisi za Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandaoni Tanzania (JUMIKITA) zilizopo jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo ya siku moja, Mwenyekiti wa ZONA, Ali Seif, akiwa ameongozana na wajumbe Rashid Ali na Khamis Hulela, walikutana na Mwenyekiti wa JUMIKITA, Shabani Matwebe, kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na jumuiya hiyo.
Social Plugin