Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema tayari vyombo vya dola vimeshawatia nguvuni watuhumiwa wa ubakaji na ulawiti wa msichana anayedaiwa kuwa ni mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam.
Agosti 4, 2024 zilisambaa video katika mitandao ya kijamii zikiwaonyesha vijana watano wakimbaka na kumlawiti binti huyo, huku wakimtuhumu kwa kile kilichosikika katika video hiyo kuwa ametembea na mume wa mtu.
Kadhalika, katika video hiyo inayodaiwa kuchukuliwa na vijana hao, binti huyo alisikika akieleza anakotokea na kumwomba msamaha mtu aliyetambulishwa kwa jina la afande.
Masauni amethibitisha kutiwa nguvuni kwa vijana hao leo, Jumanne Agosti 6, 2024 alipotafutwa na chanzo cha habari hii kwa njia ya WhatsApp.
Katika ujumbe mfupi aliotumiwa kuulizwa iwapo watuhumiwa hao wameshakamatwa, Masauni alijibu kwa kuandika "tayari' kupitia ujumbe huohuo wa njia ya WhatsApp.
Social Plugin